Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yafananisha hotuba ya Trump na mbwa anayebweka

Korea Kaskazini imejibu hotuba ya rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alibaini hadharani katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba ataisambaratisha Korea Kaskazini kama itahitajika kwa usalama wa Marekani na washirika wake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakati wa jaribio la kombora la masafa marefu Hwasong-14 lililofyatulia Julai 4 juillet 2017.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakati wa jaribio la kombora la masafa marefu Hwasong-14 lililofyatulia Julai 4 juillet 2017. KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini kupitia waziri wake wa mambo ya Nje, Ri Yong-ho, imeifananisha hotuba ya Trump na sauti ya mbwa anayebweka.

"Ikiwa Bw Trump anafikiri kuwa atatusambaratisha kwa sauti ya mbwa anayebweka basi hiyo kwake ni ndoto, " amesema Bw Yong-hi.

Marekani na Korea Kaskazini wanaendelea katika vita vya maneno, huku Korea Kaskazini ikindelea na mpango wake wa nyuklia na kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Bwana Yog-hi anatarajiwa kutoa hotuba yake kwa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.