Pata taarifa kuu
MAREKANI-UN-KOREA KASKAZINI-IRAN-USALAMA

Donald Trump azionya Korea Kaskazini na Iran

Katika hotuba yake ya kwanza kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, rais wa Marekani Donald Trump ameyashtumu "mataifa ya kijinga" ambayo yanasitisha dunia, ikiwa ni pamoja na Iran na Korea Kaskazini, ambazo amezitishia "kuzisambaratisha".

Donald Trump katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 19, 2017.
Donald Trump katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 19, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump ameonya kuwa Marekani itaangamiza Korea kaskazini iwapo italazimika kujitetea ama kuwalinda washirika wake

Wakati ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alifungua mkutano kwa kuomba kuwepo kwa ulimwengu usio na silaha za nyuklia na ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro wa Korea, rais wa Marekani ameshambulia kwa maneno makali "utawala wa kiimla" wa Pyongyang. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un yuko katika"harakati ya kujitoa muhanga", rais wa Marekani amesema kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumanne hii Septemba 19, akimuita kiongozi wa Korea Kaskazini "mtu ambaye hajafunguka" .

Wakatti huo huo rais Trump amesema Iran ni nchi ya kifisadi na inayoongozwa kidikteta kwa lengo la kutaka kuyumbisha eneo la mashariki ya kati.

Ameitaka Iran kusitisha mara moja kusaidia ugaidi mbali na kuukosoa utawala wa rais Obama kuhusu makubaliano ya mpango wa amani wa nyuklia wa taifa hilo ambao ameutaja kuwa wa aibu.

Muda umewadia kwa dunia nzima kujiunga na si kwa kuitaka serikali ya Iran kuacha kuchochea kifo na uharibifu.

Hii ni hotuba yake ya kwanza kwa viongozi wa dunia baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani mwaka uliopita.

Trump amekuwa akikosoa utendakazi wa Umoja wa Mataifa kwa matumizi makubwa ya fedha bila ya kutatua changamoto mbalimbali za dunia kama ukosefu wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.