Pata taarifa kuu
IRAN-UN-MAREKANI-USALAMA

Iran yafutilia mbali hotuba ya Trump

Iran imefutilia mbali hotuba ya rais wa Marekani Donald Trump aliyoitoa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New york.

Rais wa Irán, Hassan Rouhani.
Rais wa Irán, Hassan Rouhani. ®REUTERS/Faisal Mahmood/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Iran imesema haitishwi na kauli za rais Donald Trump na itaendelea na mpango wake nyuklia kwa ajili ya usalama wake wa ndani.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amebaini kwamba Rais Donald Trump alitoa hotuba yenye chuki ya kijinga.

Rais wa Marekani ameituhumu serikali ya Iran kwamba akisema kuwa ni utawala unaojihusisha na mauaji . Hata hivyo rais Trump alisema kuwa hataheshimu makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa chini ya uongozi wa rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama.

Wakati huo huo maafisa mbalimbali wa serikali ya Iran ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif wameiita hotuba hiyo ya Rais Trump kuwa ni ya zama za kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.