Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI-USALAMA

UNSC yaitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi

Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora ambalo lilipitia anga ya Japan, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo hicho, huku likiitaka kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia.

Korea Kaskazini ikifanya jaribio la kombora lake.
Korea Kaskazini ikifanya jaribio la kombora lake. us department of defense - reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.

Nchini Japan jeshi halikuweza kulipua kombora hilo lililopitia kwenye anga yake.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha NHK, jeshi la Japani halikuweza kuharibu kombora baada ya kuliona. Hata hivyo, serikali ilipendekeza kuwa haitasita kufanya hivyo ikiwa kombora au kifaa chochote kile kutoka Korea Kaskazini kitapita juu ya anga yake.

Itakubuka kwamba, Japan na Marekani, katika pwani ya rasi ya Korea, wana mfumo wa kujikinga dhidi ya maokombora kwenye ardhi na baharini katika nchi ote hizo mbili.

Ni jaribio la 13 la Korea Kaskazini mwaka huu pekee. Siku ya Jumamosi iliyopita Pyongyang ilirusha makombora matatu ya masafa mafupi katika Bahari ya Japan. Hakuna hata mmoja miongoni mwa makombora hayo yalikua tishio kwa Marekani au kwa eneo la Marekani la Guam.

Lakini tukio la siku ya Jumanne linaonyesha uwezekano wa kuongezea kwa mvutano katika ukanda huo, wakati ambapo Pyongyang ilitishia kurusha kwa mfululizo makombora kuelekea eneo la Marekani la Guam. Kombora ambalo lingeweza kupta juu ya anga ya Japan.

"Ulimwengu umepokea ujumbe wa mwisho kutoka Korea Kaskazini: serikali imeonyesha dharau yake kwa majirani zake, kwa wanachama wote wa Umoja wa Mataifa na kwa viwango vya chini vya tabia zinazokubalika kimataifa," alisema rais wa Marekani Donald Trump katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe aliomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, na akitoa wito wa "kuongeza shinikizo kwa Korea ya Kaskazini, kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa."

Kwa jaribio hili, Korea Kaskazini inajibu mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka ya Marekanikwa ushirikiano na Korea Kusini. Pyongyang, inayachukulia mazoezi hayo kamauwezekano wa uvamizi dhidi yake. Labda pia ni jibu kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Japan ambayo yalimalizika hivi karibunkatika kisiwa cha Hokkaido

Waziri Mkuu wa Japan anaamini kuwa Japan, ambapo kunapatikana kambi kubwa za jeshi la Marekani nje ya Marekani, iko hatarini kwa kushambuliwa na Korea Kaskazini kama Korea ya Kusini au Marekani alisema.

Kwa mujibu wa washauri wa Shinzo Abe, Korea Kaskazini itasita kabla ya kushambulia Korea Kusini, na wala haitathubutu kushambulia Marekani. Japan, kwa upande wake, inategemea usalama wake juu ya mwavuli wa nyuklia wa Marekani.

Hata hivyo, Tokyo inajiuliza kama Marekani ingeilinda wakati wa mashambulizi ya Korea Kaskazini. Siku ya Jumanne, Pentagon ilithibitisha kombora kutoka Korea Kaskazini lilipita juu ya anga ya Japan, lakini ilibaini kwamba kombora hilo halikua na tishio lolote kwa Marekani.

Shinzo Abe alisema katika mazungumzo ya simu na Donald Trump, wawili hao walikubaliana kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini.

Baada ya miezi kadhaa ya mvutano, rais wa Marekani Donald Trump alibaini wiki iliyopita kwamba Korea Kaskazini "imeanza kuheshimu Marekani."

Siku chache baadae Pyongyang ilirusha kombora iliyoahidi kuelekea kisiwa cha Guam. Lakini siku ya Jumanne, Korea Kaskazini kurusha kombora juu ya anga ya mshirika mkuu wa Marekani katika bara la Asia, kiongozi wa Korea Kaskazini alionyesha kuwa hana hofu yoyote. Donald Trump alioonya: "Mambo yote yako kwenye meza. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.