Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-JAPAN-USALAMA

Korea Kaskazini yarusha kombora kuelekea Japan

Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora kuelekea bahari ya Japan, askari wa Korea Kusini wamebaini. Kombora hilo lilipita kwenye anga ya kaskazini mwa Japan, kwa mujibu wa serikali ya Japani, taarifa iliyothibitishwa na Pentagon.

Korea Kaskazini ilirusha kombora tarehe 29 Agosti 2017 kuelekea Bahari ya Japan, uongozi wa jeshi la Korea Kusini limebaini.
Korea Kaskazini ilirusha kombora tarehe 29 Agosti 2017 kuelekea Bahari ya Japan, uongozi wa jeshi la Korea Kusini limebaini. REUTERS/KCNA
Matangazo ya kibiashara

Jaribio hili linakuja wakati ambapo mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani yanaendelea, mazoezi ambayo Korea Kaskazini inachukulia kama tishio la moja kwa moja kwa usalama wake.

"Kombora lisilojulikana" lilirushwa kutoka Sunan karibu na Pyongyang saa 5:57 saa za Korea Kaskazini (sawa na saa siku ya Jumatatu saa 20:57 usiku saa za kimataifa), kwa mujibu wa uongozi wa jeshi la Korea Kusini. "Korea Kusini na Marekani wanatathmini kwa pamoja hali hiyo," uongozi wa jeshi la Korea Kusini umeongeza. Kombora lililorushwa na Korea Kaskazini inaonekana kuwa lilipita kwenye anga ya Japan, kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo. Kwa mujibu wa NHK, kombora hilio lilipasuka vipande vitatu na lilianguka katika pwani ya kisiwa cha Hokkaido.

Mfumo wa onyo wa mamlaka uliwashauri wakazi wa eneo hilo kuchukua tahadhari, lakini kwa mujibu wa kituo cha habari cha serikali ya Japan, hakuna hasara iliyotokea. Msemaji wa Waziri Mkuu, Yoshihide Suga, amesema kuwa kombora hilo ni "tishio kubwa kwa usalama" wa Japan.

Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.

Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.

Wakati huo huo Bwana Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote wamekubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.

Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.