Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yaapa kushambulia kisiwa cha Marekani cha Guam

Korea Kaskazini inasema imetishia kukishambulia kisiwa cha Marekani cha Guam siku za hivi karibuni, licha ya onyo la rais wa Marekani Donald Trump. Vita vya maneno kati ya Washington na Pyongyang vimeendelea.

Kim Jong-un na majenerali wake, katika mazoezi ya kijeshi, picha ya zamani iliyowekwa wazi Februari 21 mwaka 2015.
Kim Jong-un na majenerali wake, katika mazoezi ya kijeshi, picha ya zamani iliyowekwa wazi Februari 21 mwaka 2015. REUTERS/KCNA
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii Marekani iliionya Korea Kaskazini ikisema kuwa mpango wake huo wa kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam unamaanisha kuwa huo utakuwa mwisho wa utawala wa Kim Jon-un.

Waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis alisema kuwa Korea Kaskazini itashindwa ikiwa itaingia vitani na Marekani.

Wakati huo huo Korea Kaskazini ilipuuzna onyo la rais wa Marekani Donald Trump kuwa itaishambuliwa vikali.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Korea Kaskazini, makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Marekani cha Guam.

Mpango huo utatekelezwa baada ya kuidhinishwa na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, vyanzo vya usalama vimebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.