Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini: Tuko tayari kurusha makombora karibu na kisiwa cha Marekani

Korea Kaskazini imetangaza kwamba inatathmini uwezekano wa kufanya jaribio jingine la kurusha makombora karibu na jimbo la Marekani la Guam katika bahari ya Pasifiki, kwa mujibu wa Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini.

Korea ya Kaskazini yatishia kurusha makombora karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.
Korea ya Kaskazini yatishia kurusha makombora karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam. REUTERS/KCNA
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema jeshi la nchi hiyo "linachunguza kwa makini mpango wa kuanzisha moto wa kuzingira Guam kwa kutumia makombora ya roketi ya masafa ya wastani na ya masafa marefu ya Hwasong-12".

Korea Kaskazini imechukua uamuzi huo, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuionya nchi hiyo kwamba itakabiliwa na mkono wa chuma. Taarifa hii inaashiria kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili.

Rais Trump ametoa onyo hilo baada ya ripoti kwenye vyombo vya habari kusema kwamba Korea Kaskazini imeweza kuunda kichwa cha silaha za nyuklia chenye uwezo wa kutosha kwenye makombora yake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap , mpango huu utawasilishwa kwa viongozi wakuu baada ya "kutathminiwa kwa kina na kukamilishwa" na utatekelezwa kiongozi wake Kim Jong-un akiamrisha,

Taarifa ya gazeti la Washington Post, ikunukuu maafisa wa ujasusi wa Marekani, imedokeza kwamba Korea Kaskazini inaunda silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kasi zaidi ya iliyotarajiwa.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa uliidhinisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini.

Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.