Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Vita vya maneno vyaongezeka kati ya Korea Kaskazini na Marekani

Baada ya Korea Kaskazini kuzindua kombora lake la kwanza la masafa marefu linalokwenda hadi bara jingine siku ya Jumanne, tarehe 4 Julai, Washington na Pyongyang wameingia katika vita vya maneno.

Picha iliotolewa na shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA ambapo rais Kim Jong-un akifurahia baada ya jaribio la kombora la masafa marefu linalokwenda hadi bara jingine tarehe 4 Julai, 2017.
Picha iliotolewa na shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA ambapo rais Kim Jong-un akifurahia baada ya jaribio la kombora la masafa marefu linalokwenda hadi bara jingine tarehe 4 Julai, 2017. KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Marekani imeshutumu "kuongezeka kwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia" na kuomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa upande wake, rais wa Korea Kaskazini alisema jaribio hilo lilikuwa "zawadi" kwa Siku Kuu ya taifa ya Marekani.

Taarifa ya kwanza ya Pentagon ya siku ya Jumanne asubuhi, ilibaini kwamba jaribio hilo lilikua la kombora la masafa ya wastani. Kombora la Korea Kaskazini lilikaa hewani kwa muda wa dakika 37 kabla ya kuanguka katika bahari ya Japan. Lakini madai ya wataalamu yalibadilika mchana, na kusema kuwa halikua jaribio la kombora la masafa ya wastani bali la masafa marefu, amearifu mwandishi wetu nchini Marekani, Anne-Marie Capomaccio.

"Kuongezeka kwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia"

Wakati huo huo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson alithibitisha taarifa hiyo, huku akilaani "kuongezeka kwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia". Bw Tillerson alisema kwa hakika jasribio hilo lilikua la kombora la ICBM la masafa marefu linalokwenda hadi bara jingine.

Bwana Tillerson pia alionya kwamba taifa lolote ambalo linasaidia kiuchumi na kijeshi Korea kaskazini ama limefeli kuidhinisha kwa ukamilifu maamuzi ya baraza la usalama ya Umoja wa Mataifa linasaidia utawala hatari.

Korea Kaskazini imepiga hatua katika makombora ya aina hiyo ambayo yanaweza kufika hadi Alaska, nchini Marekani.

Kwa upande wake, Jumatano hii asubuhi, shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA limearifu kwamba rais Kim Jong-un, ambaye alisimamia zoezi hilo, alisema kuwa jaribio hilo lilikuwa ni "zawadi" kwa "Wanaharamu Wamarekani" kwa Siku Kuu ya yao ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.