Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani na Korea Kaskazini watishia kuishambulia Korea Kaskazini

Marekani na Korea kusini zimetishia kuishambulia Korea Kaskazini kutokana uamuzi wa taifa hilo kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu la ICBM siku ya Jumanne.

Rais Donald Trump na mwenmzake wa Korea Kusini Jae-Moon wametishia kuishambulia Korea Kaskazini
Rais Donald Trump na mwenmzake wa Korea Kusini Jae-Moon wametishia kuishambulia Korea Kaskazini REUTERS/Jim Bourg
Matangazo ya kibiashara

Onyo hilo linajiri wakati ambapo mataifa hayo mawili yamefanya zoezi la pamoja la kijeshi la makombora ya masafa marefu.

Baada ya jaribio hilo, waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson aliionya Pyongyang kwamba inaendeleza vitisho dhidi ya Marekani na dunia nzima kwa jumla.

Maafisa wawili wakuu kutoka Mareani na Korea Kusini wamesema kuwa kujizuia ni chaguo lao na kubaini kwamba hatua hiyo inaweza kubadilika wakati wowote.

Wamesema kuwa hawatokubali kukaa kimya bila kufikiria kuchukua hatua kali.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa jaribio hilo la kombora la masafa marefu ni zawadi kwa Wanaharamu Wamarekani wakati wa siku kuu yao ya uhuru, kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.