Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-UN-USHIRIKIANO

UN yaomba Pyongyang kusitisha majaribio yake ya makombora

Umoja wa Mataifa umeomba Korea Kaskazini "kusitisha mara moja majaribio yake ya makombora ya masafa marefu ambayo" yanatishia usalama wa ukanda na wa kimataifa."

Raia wa Korea Kaskazini wakiangalia kupitia televisheni habari kuhusu kurushwa kwa kombora la masafa marefu, Mei 22, 2017 katika mji wa Pyongyang.
Raia wa Korea Kaskazini wakiangalia kupitia televisheni habari kuhusu kurushwa kwa kombora la masafa marefu, Mei 22, 2017 katika mji wa Pyongyang. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ni wazi kuwa Korea ya Kaskazini inapinga maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiendelea kwa kasi na shughuli zake za kurusha makombora ya masafa marefu," msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema Jumatatu hii Mei 22, 2017 katika kukabiliana na majaribio ya makombora ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini.

Pyongyang pia inapaswa "kufikiria kuanza mazungumzo yanayofaa."

Korea ya Kaskazini imesema siku Jumatatu kuwa ilifaulu kurusha kombora la masafa ya wastani licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Maazimio ya Umoja wa Mataifa yanapiga marufuku shughuli yoyote ya nyuklia au jaribio lolote la kombora la masafa marefu, na Pyongyang inakabiliwa na mfululizo wa vikwazo vya kiuchumi ambavyo Marekani inataka hasa kuongezea.

Kwa ombi la Washington, Seoul na Tokyo, kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimepangwa kufanyika Jumanne hii Mei 23.

Washington pia inafanya mazungumzo na Beijing, mshirika mkuu wa Pyongyang, kuhusu azimio jipya la kuongeza shinikizo kwa serikali ya kikomunisti ya Pyongyang.

Korea ya Kaskaziniimefanya majaribio kadhaa ya makombora tangu mwanzoni mwa mwaka huu na imepiga hatua kubwa katika jitihada zake za kuendeleza kombora la masafa marefu kutoka bara moja kwenda bara jingine, kombora ambalo linajulikana kwa jina la ICBM, lenye uwezo wa kubeba mashambulizi ya nyuklia katika bara la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.