Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Nikki Haley: Tunawaonya washirika wa Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilijadili siku ya Jumanne katika kikao cha faragha kuhusu vikwazo vikali dhidi ya Korea Kaskazini na marufuku kwa mipango yake ya nyuklia na makombora ya masafa marefu, baada ya jaribio jipya la makombora mwishoni mwa wiki iliyopita.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, amwataka washirika wa Korea Kaskazini kuachana na mpango wao wa kuiunga mkono nchi hiyo.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, amwataka washirika wa Korea Kaskazini kuachana na mpango wao wa kuiunga mkono nchi hiyo. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Marekani na China vinaanda azimio jipya kwa ajili ya hatua za kuichukulia vikwazo vya ziada nchi ya Korea Kaskazini, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley ametangaza mbele ya vyombo vya habari.

"Sote tunapaswa kuionya Korea Kaskazini:" Inatosha. Hakuna mchezo. Ni hatari, " alisisitiza Bi Haley, akionya nchi ambazo hazitatekeleza vikwazo vilivyochukuliwa mwongo mmoja uliyopita kwamba zitakumbwa na ulipizaji kisasi kutoka Marekani.

Kabla ya kuingia katika kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Nikki Haley alisema nchi yake na China, mshirika katika masuala ya kijeshi na kidiplomasia wa Korea ya Kaskazini, wanaanda vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.