Marekani yaionya Korea Kaskazini
Katika mahojiano na shirika la habari la ABC, Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert Raymond McMaster Jeneral Mc Master amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu na Korea Kaskazini.
Imechapishwa:
Herbert Raymond McMaster amesisitiza kuwa majaribio ya makombora ya hivi karibuni, yanaonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini, huku akibaini kuwa kuna makubaliano ya kimataifa, ikiwemo China, kuhakikisha tabia hii haiendelei.
Herbert Raymond McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China.
Wakati huo huo Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, ambaye anazuru Korea Kusini amesema uhuru utashinda.