Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yashindwa katika jaribio jipya la kombora

Jaribio jipya lakombora la Korea Kaskazini limeshindwa wakati lilipolipuka baada ya uzinduzi leo Jumapili, jeshi la Marekani limesema, siku moja baada Pyongyang kwa jeuri kuonesha shehena yake ya silaha wakatiwa gwaride kubwa la kijeshi.

Magari ya kijeshi yakiwa yamebeba makombora wakati wa gwaride  kuadhimisha miaka105 mwanzilishi wa taifa hilo , Kim Il Sung mjini  Pyongyang, Korea  Kaskazini April 15, 2017.
Magari ya kijeshi yakiwa yamebeba makombora wakati wa gwaride kuadhimisha miaka105 mwanzilishi wa taifa hilo , Kim Il Sung mjini Pyongyang, Korea Kaskazini April 15, 2017. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Kushindwa huku ambako kunaweza kuonekana kama jambo la aibu kwa serikali mbele ya umma, kumetokea huku kukiwa na kuongezeka kwa mvutano katika kanda kuhusu lengo la Korea kuwa na silaha nzito za nyuklia.

Korea ya Kaskazini imeonesha silaha zake za kivita leo Jumamosi mjini Pyongyang wakati kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un akikagua gwaride la heshima kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa babu yake marehemu Kim Il-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo, na kuahidi kuwa tayari kujibu shambulizi lolote la nyuklia.

Mvutano kuhusu lengo la Korea Kaskazini kuwa na silaha nzito za Nyuklia umekuwa katika kipimo baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kupeleka manuari ya kijeshi katika rasi ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.