Pata taarifa kuu
URUSI-AJALI

Ndege ya jeshi la Urusi: kisanduku cheusi chapatikana, zoezi la kutafuta miili laendelea

Zoezi kabambe lililoendeshwa katika bahari ya Nyeusi baada ya ajali ya ndege ya kijeshi lilipelekea kupatikana kwa moja ya visanduku vya sauti vya ndege hiyo Jumanne hii Desemba 27. Kisanduku hiki ni kifaa muhimukwa kujua sababu ya ajali ya ndege hiyo. Ajali ambayo ilitokea siku kadhaa kabla ya mwisho wa Mwaka.

Zoezi la kutafuta kisanduku cha sauti na miili ya watu waliokuwemo katika ndege ya kijeshi ya Urusi Tupolev Tu-154, laendelea katika bahari Nyeusi.
Zoezi la kutafuta kisanduku cha sauti na miili ya watu waliokuwemo katika ndege ya kijeshi ya Urusi Tupolev Tu-154, laendelea katika bahari Nyeusi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kisanduku hiki kilipatikana saa 8:42 saa za kimataifa kwenye kina chenye umbali wa mita 17 na mita 1,600 kutoka pwani, karibu na mji wa Sochi ambapo ndege hiyo ilitokea ikipaa hewani. "Kifaa hiki muhimu cha kurikodi sauti kilipelekwa mjini Moscow mchana kwa uchunguzi zaid, " Wizara ya Ulinzi imetangaza.

Kisanduku cha chuma ambacho ndani yake kunapatikana kifaa cha kurekodi data za ndege "kiko katika hali ya kuridhisha," Wizara ya Ulinzi ilisema.

Serikali ya Urusi imefutilia mbali madai ya shambulizi kama sababu ya ajali ya ndege hiyo aina ya Tupolev Tu-154, ambayoilianguka Jumapili muda mfupi baada ya kuruka kuelekea Syria, ikiwa na watu 92 ambao ni pamoja na zaidi ya wanamuziki 60 wa jeshi la Urusi.

Kama vibande kadhaa vya ndege vilipatikana, basi kupatikana kwa visanduku vyeusi ni hatua muhimu ili kujua mlolongo wa matukio. Kwa mujibu wa chanzo kilichonukuliwa na shirika la habari la Interfax, kifaa kilichopatikana ni kile kinachohifadhi vigezo vya kiufundi vya ndege, kisandukuchenye sauti hakijapatikana.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi, zoezi la kutafuta kisanduku cheusi kingine pamoja na miili ya watu waliokuwemo, linaendelea. "Mpaka sasa miili 12 na vipande 156 vya ndege hiyo vimepatikana," jeshi limesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.