Pata taarifa kuu
LEBANON-SYRIA-VITA-ATHARI-UCHUMI-USALAMA

Lebanon : uharibifu unaosababishwa na mgogoro wa Syria

Lebanon iimekumbwa hali ngumu kutokana na vita inayoendelea nchini Syria. Lebanon inakabiliwa na hali hiyo hasa na uwepo wa wakimbizi milioni 1.2 wa Syria, sawa na theluthi moja ya wakazi wake.

Mageri ya kijeshi ya Libanon yakiingia katika mji wa Ersal, Jumamosi, Agosti 2.
Mageri ya kijeshi ya Libanon yakiingia katika mji wa Ersal, Jumamosi, Agosti 2. AFP PHOTO / STR
Matangazo ya kibiashara

Lakini hili si tatizo linaloathiri tu nchi hiyo. Lebanon inakabiliwa pia na mashambulizi wanajihadi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Paul Khalifeh, wanajihadi wamepeleka kwenye mpaka wa Lebanon na Syria, mashariki mwa Lebanon, wapiganaji 3,000 katika eneo la kilomita mraba 500, sawa na asilimia 5 ya aridhi yake. Kundi la wapiganaji wa dola la Kiislamu na Al-Nusra Front, tawi la Al-Qaeda nchini Syria, wanagawana kudhibiti mkoa huu wenye milima, ambayo ina urefu wa mita 2700 kwenda juu.

Jeshi la Lebanon limepeleka kwenye eneo hilo wanajeshi 5000, wakisaidiwa na vifaru vya kijeshi na silaha za kivita pamoja na helikopta za kivita. Mamia ya Hezbollah na wapiganaji na vikundi vya kijeshi, hasa vinavyoundwa na wanakijiji, pia wanashiriki katika ulinzi wa mkoa huo.

Wanajihadi wamekua wakiendesha mashambulizi dhidi ya ngome za jeshi ili kuwa kwenye mtari wa mbele wa kupata silaha na kujaribu kudhibiti vijiji vya Lebanon. Tangu Agosti mwaka 2014, jeshi limepoteza zaidi ya wanajeshi sitini huku zaidi ya 20 wakijeruhiwa katika mapigano dhidi ya watu wenye msimamo mkali.

Jeshi la Lebanon lilipata hivi karibuni idadi kubwa ya silaha zilizotolewa na Marekani, na kwa sasa inasubiri mwezi Aprili, utekelezaji wa mkataba wa dola bilioni 3 wa mauzo ya silaha kutoka Ufaransa, pesa ambazo zitalipwa na Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.