Pata taarifa kuu
CHINA-VIFO-USALAMA

Mwaka Mpya China: watu 35 wafariki Shanghai

Watu 35 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa mjini Shanghai nchini China baada ya kukanyagana wakati wa kuupokea mwaka mpya wa 2015.

Kukanyagana kumesababisha vifo vya watu 35 katika mji wa Shanghai, usiku wa tarehe 31 Desemba mwaka 2014 kuamkia tarehe 1 janvier mwaka 2015.
Kukanyagana kumesababisha vifo vya watu 35 katika mji wa Shanghai, usiku wa tarehe 31 Desemba mwaka 2014 kuamkia tarehe 1 janvier mwaka 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika katika viwanja vya Chenyi katika mji huo mkubwa nchini China kuukaribisha mwaka mpya wakati mkasa huo ulipotokea.

Ripoti zinaeleza kuwa watu hao walikangayangana wakati wakipigania kupokea fedha zinazoelezwa kuwa mbovu zilizorushwa kutoka jengo moja la burudani.

Picha katika mitandao ya kijamii kutoka eneo hili zinaonesha watu wakipokea huduma ya kwanza na polisi wakizingira viwanja hivyo.

Rais Xi Jinping amesema amesikitishwa na mkasa huo na kuagiza uongozi wa Shanghai kuchunguza na kubaini ukweli kuhusu kilichotokea.

Uongozi wa mji wa Shanghai unasema waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali wanakopata matibabu.

Inaelezwa kuwa zaidi ya watu Laki tatu walihudhuria maadhimisho hayo ya mwaka mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.