Pata taarifa kuu
CHINA-HAKI ZA BINADAMU-SHERIA

China: kesi ya mwandishi wa habari Gao Yu yasikilizwa

Kesi ya mwandishi wa habari, Gao Yu imeanza kusikilizwa leo Ijumaa Novemba 21 nchini.Gao Yu maarufu" shujaa kwa uhuru wa vyombo vya habari" mwaka 200. Mwandishi huyo wa habari ameripoti mahakamani leo Ijumaa Novemba 21, mjini Pekin.

Mwandishi wa habari, raia wa China, Gao Yu wakati wa mkutano na vyombo vya habari, Februari mwaka 2007.
Mwandishi wa habari, raia wa China, Gao Yu wakati wa mkutano na vyombo vya habari, Februari mwaka 2007. AFP PHOTO/MIKE CLARKE
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutoweka Aprili 24 mwaka 2014, majuma kadhaa kabla ya maadhimisho ya miaka 25 ya mauaji yaliyotokea Tiananmen, Gao Yu alionekana hadharani mwezi mmoja baadaye kwa kukiri kufedheheshwa mbele ya kamera. Sasa amerudi na kauli ile ile ya kufedheheshwa.

Akivalia sare za wafungwa, Gao Yu, alionyeshwa mbele ya kamera ya televisheni ya serikali mwezi Mei.

Gao Yu, ambaye alipata umaarufu mkubwa kufuatia mapambano aliyoendesha juu ya kutetea haki za binadamu, amebaini kwamba licha ya kudhalilishwa, na kwenda kinyume na maadili ya taaluma ya uandishi, ataihakikishia Mahakama kuwa hana hatia.

Gao Yu, kupitia mwanasheria wake, Mo Shaoping, amekiri kuwa alivunja sheria na kutishia maslahi ya kitaifa.

" Gao Yu, amesema wazi kwamba polisi ilimshawshi kwa kumfanyia vitisho mtoto wake. Gao Yu amebaini kwamba alilazimishwa kusema uongo wakati alipokua akirekodiwa. Kwa hiyo aliyoyazungumza wakati huo yanapaswa kufutwa, kwani ni ushahidi usiyo na ukweli. Jambo la pili Gao Yu, amekanusha tuhuma dhidi yake kwamba alihatarisha usalama wa taifa kwa kosa la uhaini. Jambo la tatu, afya ya Gao Yu si nzuri. Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 70. Ana magonjwa mengi na anapaswa kutumia dawa. Ameniambia kuwa alipoteza fahamu mara kadhaa sehemu anakozuiliwa", Mo Shaoping, amesema.

Gao Yu anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela iwapo atapatikana na hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.