Pata taarifa kuu

Haiti: Jimmy Chérizier almaarufu "Barbecue", ni nani?

Amekuwa anachochea ugaidi kwa miaka mingi nchini Haiti na kwa sasa anaonekana waziwazi kama kiongozi wa mapinduzi yanayotaka kumwondoa Waziri Mkuu madarakani. Jimmy Chérizier, aliyepewa jina la utani "Barbecue", ametishia kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vitasababisha mauaji ya halaiki ikiwa Ariel Henry hatajiuzulu. Je! ni nani kiongozi huyu wa genge, afisa wa zamani wa polisi mwenye umri wa miaka 46?

Jimmy “Barbecue” Chérizier, mjini Port-au-Prince, Machi 5, 2024.
Jimmy “Barbecue” Chérizier, mjini Port-au-Prince, Machi 5, 2024. AFP - CLARENS SIFFROY
Matangazo ya kibiashara

 

Wengine humwita "mtu mwenye nguvu zaidi nchini Haiti." Na kwa sasa, hali hii haiko mbali na ukweli. Vurugu zinazochochewa na watu wake zinamzuia Waziri Mkuu kurejea nchini, na hivyo kusababisha ombwe la madaraka ambalo Jimmy Chérizier anakusudia kuchukua fursa hiyo.

Afisa huyu wa zamani wa polisi ndiye kiongozi wa magenge yenye nguvu zaidi, yanayoitwa "G9 na Familia". Pia hapendi neno genge na anapendelea kuzungumzia "kundi lenye silaha". Bado, "G-9 na familia" inahusika kwa kiasi kikubwa na vurugu ambazo nchi imeingia tangu mwaka 2020.

Msaada kutoka kwa mamlaka

Kufuatia mauaji ya Rais wa zamani Jovenel Moïse mnamo mwezi wa Julai 2021, Jimmy Chérizier alitoa wito wa mapinduzi dhidi ya wasomi wa kisiasa wa nchi hiyo, wasomi ambao baadhi ya wanachama hata hivyo walimuunga mkono katika shughuli zake za uhalifu. Kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Moïse na sehemu ya polisi walimpa pesa na silaha. Akiwa na watu wake, alidhibiti haswa vitongoji duni vya mji mkuu, na tabia ya wengi dhidi ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.