Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Ghasia nchini Haiti: Kiongozi wa genge mwenye ushawishi atishia 'vita vya wenyewe kwa wenyewe'

Kiongozi wa genge la Haiti mwenye ushawishi mkubwa ametishia "vita vya wenyewe kwa wenyewe" vya umwagaji damu siku ya Jumanne ikiwa Waziri Mkuu Ariel Henry atasalia madarakani, huku nchi hiyo ndogo na maskini ya Caribbean ikikabiliwa na ghasia kubwa.

Afisa wa zamani wa polisi Jimmy "Barbecue" Cherizier, kiongozi wa muungano wa "G9", anaongoza maandamano dhidi ya Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry, huko Port-au-Prince, Haiti, Septemba 19, 2023.
Afisa wa zamani wa polisi Jimmy "Barbecue" Cherizier, kiongozi wa muungano wa "G9", anaongoza maandamano dhidi ya Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry, huko Port-au-Prince, Haiti, Septemba 19, 2023. REUTERS - RALPH TEDY EROL
Matangazo ya kibiashara

Magenge hayo, ambayo yanadhibiti maeneo yote ya Haiti na mji mkuu, yalitangaza wiki iliyopita kwamba yanafanya masambulizi dhidi ya serikali na tangu wakati huo yamefanya mashambulizi dhidi ya miundombinu na maeneo ya kimkakati, yakitumia fursa ya safari nje ya nchi ya Waziri Mkuu.

"Ikiwa Ariel Henry hatajiuzulu, ikiwa jumuiya ya kimataifa itaendelea kumuunga mkono, tunaelekea moja kwa moja kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vitasababisha mauaji ya halaiki", alitishia siku ya Jumanne Jimmy ChΓ©rizier, aliyepewa jina la utani "Barbecue", wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, ambao ulimweka chini ya vikwazo, afisa huyo wa zamani wa polisi mwenye umri wa miaka 46 ni mmoja wa viongozi wa magenge wenye ushawishi mkubwa, na anaongoza muungano wa magenge yenye silaha yanayoitwa "familia ya G9" na washirika wake.

Magenge haya yanatoa wito wa kumpindua Ariel Henry, aliye madarakani tangu kuuawa kwa Rais Jovenel MoΓ―se mwaka wa 2021, na ambaye alipaswa kuondoka madarakani mwanzoni mwa mwezi wa Februari.

"Lazima tuungane. Ama Haiti iwe paradiso yetu sote, au jehanamu kwetu sote," alitangaza Bw. ChΓ©rizier, akiwa na fulana ya kuzuia risasi na kubeba silaha na kuzungukwa na watu waliojifunika nyuso.

Mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince umekuwa chini ya hali ya hatari na sheria ya kutotoka nje tangu siku ya Jumapili, baada ya kuachiliwa kwa maelfu ya wafungwa na magenge yenye silaha.

Ashindwa kurudi Port-au Prince

Waziri Mkuu alikwenda Nairobi wiki jana kutia saini makubaliano ya kutuma maafisa wa polisi wa Kenya nchini Haiti kama sehemu ya ujumbe wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Marekani.

"Alitua Puerto Rico" siku ya Jumanne, msemaji wa serikali ya Puerto Rico, Sheila Anglero aliliambia shirika la habari la AFP kwa simu jioni. Kisha akafafanua kuwa hakujua ikiwa bado yuko kisiwani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.