Pata taarifa kuu

Haiti: Serikali yatangaza hali ya hatari na sheria ya kutotoka nje usiku Port-au-Prince

Hali ya hatari imetangazwa nchini Haiti, baada ya wikendi yenye vurugu hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince na viunga vyake. Magenge yenye silaha yalishambulia magereza mawili. Maelfu ya wafungwa walitoroka; angalau watu kumi walifariki. Sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa ili kupata tena udhibiti wa mji mkuu wa Port-au-Prince. Hali hii inapaswa kudumu angalau saa 72.

Haiti inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa, usalama na kibinadamu tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse mnamo 2021.
Haiti inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa, usalama na kibinadamu tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse mnamo 2021. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Msururu wa ghasia unaendelea nchini Haiti. Hali ya hatari na sheria ya kutotoka nje imetangazwa baada ya ghasia za wikendi hii katika jimbo nzima la magharibi kwa muda wa saa 72. Marufuku ya kutotoka nje hutangazwa katika eneo hili kati ya saa 12 hadi saa 11 alfajiri Jumatatu, Jumanne na Jumatano, na Jumapili kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 11 alfajiri, inabaini taarifa ya serikali kwa vyombo vya habari.

Waziri wa Uchumi na Fedha, Patrick Michel Boisvert, ndiye aliyetia saini taarifa ya serikali kwa vyombo vya habari bila kuwepo Waziri Mkuu Ariel Henry, ambaye yuko ziarani nchini Kenya. Hii inaashiria kwamba matangazo haya yanakuja kufuatia kuzorota kwa usalama nchini, hasa huko Port-au-Prince, "na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na magenge yenye silaha", pamoja na kutilia maanani "kutoroka kwa wafungwa hatari", vitendo "vya kuhatarisha usalama wa taifa" kulingana na serikali.

Mwishoni mwa wiki hii, kwa kweli, karibu watu kumi walikufa na maelfu ya wafungwa walitoroka jela kuu la mji mkuu, wakati wa operesheni iliyohusishwa magenge yenye silaha.

Katika hali hii ya vurugu, huduma za afya zinajaribu, kadri wawezavyo, kuendelea kufanya kazi. Hivi ndivyo hali ya hospitali ya Tabarre, inayosimamiwa na shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, RSF, huko Port-au-Prince. Taasisi hiyo inakaribisha watu zaidi na zaidi waliojeruhiwa katika siku za hivi karibuni: "Wagonjwa wote wanaofika wana majeraha mengi ya kisaikolojia. Tunapokea hata wagonjwa katika hospitali zetu ambao hawatokani na jukwaa letu la kiufundi kwa sababu hawana mahali pa kwenda. Na jana usiku, tulikuwa na wajawazito waliojitokeza hospitalini na kuhitaji kujifungua. Hawana mahali pa kwenda, hivyo wanakuja kwetu,” anabainisha Mumuza Muhindo, mkuu wa misheni ya MSF nchini Haiti, afisa wa hospitali ya Tabarre.

"Athari nyingine ni wasiwasi kuhusu dawa. Meli za mizigo zimezuiwa bandarini. Hatuwezi kuipata. Tunatumai kwamba, haraka, kutakuwa na utulivu ambao ungeturuhusu kupata dawa hizi, kwa sababu vinginevyo tunaogopa uhaba, ambao utaharibu uwezo wetu wa kujibu huduma bure kwa idadi ya watu. Idadi ya wagonjwa inaongezeka siku baada ya siku,” anaeleza Mumuza Muhindo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.