Pata taarifa kuu

Brazil: Watu 14 wafariki katika ajali ya ndege Amazon

Watu 14 wamefariki katika ajali ya ndege huko Barcelos, mji wa kitalii katika eneo la Amazon nchini Brazil, gavana wa jimbo la Amazonas Wilson Lima ametangaza. Abiria kumi na wawili na wahudumu wawili walikufa katika ajali hii, Bw. Lima ameandika kwenye X (zamani ikitwa Twitter).

Watu wakitazama ndege iliyoanguka kwenye miti mikubwa, huko Barcelos, jimbo la Amazonas, Brazil mnamo Septemba 16, 2023.
Watu wakitazama ndege iliyoanguka kwenye miti mikubwa, huko Barcelos, jimbo la Amazonas, Brazil mnamo Septemba 16, 2023. © STRINGER / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Watu 14 waliuawa Jumamosi katika ajali ya ndege huko Barcelos, mji wa kitalii katika Amazon nchini Brazil, kulingana na mamlaka. Ndege hiyo, yenye injini mbili ya turboprop EMB-110 iliyotengenezwa na kampuni ya kutengeneza ndege ya Brazil Embraer, ilikosa kutua Barcelos kutokana na mvua kubwa, Katibu wa Usalama wa Jimbo la Amazonas Vinicius Almeida amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Ndege hiyo ilipoteza njia baada ya kutua mbali sana na kuwaua abiria wote 12 na wahudumu wawili. Hakuna manusura, amesema Vinicius Almeida. Kulingana na vipengele vya kwanza vya uchunguzi, abiria wote walikuwa wanaume, raia wa Brazil ambao walikuwa wakienda katika eneo hilo kwa ajili ya michezo ya uvuvi, serikali ya jimbo imesema katika taarifa.

Picha zilizorushwa na vyombo vya habari vya Brazil zimeonyesha ndege hiyo ndogo nyeupe ikiwa imedondoka kwenye barabara ya udongo, sehemu ya mbele ya ndege hiyo ikiwa imeangukia sura ya mbele kwenye miti minene.

Vipimo vya kisayansi

Ndege hiyo iliondoka Manaus, mji mkuu wa jimbo hilo, kuelekea Barcelos, safari ya takriban dakika 90. Kulingana na mamlaka, ndege nyingine mbili zilizokuwa zikikaribia Barcelos wakati huo huo zilirejea Manaus kutokana na hali mbaya ya hewa. Uchunguzi ulikabidhiwa kwa Jeshi la Anga na polisi, mamlaka imesema. Barcelos ambayo inapatikana kwenye eneo la Rio Negro, tawimto la Amazon, inapakana na mbuga kadhaa za kitaifa.

Kulingana na mamlaka, miili ya wahanga itasafirishwa hadi mji mkuu wa jimbo siku ya Jumapili kwa utambuzi. Haikuwezekana kufanya hivyo mapema kwani safari za usiku hazijaruhusiwa katika eneo hilo. "Ndege ya jeshi la anga ilitazamiwa kuondoka Manaus leo karibu saa kumi na moja alfajiri na wachunguzi na maafisa wa idara ya huduma ya dharura," Vinicius Almeida amesema. "Tunatumai kuwa na uwezo wa kurudisha miili hiyo Manaus na kuiwasilisha mara moja kwa uchunguzi wa kitaalamu kabla ya kuitoa kwa familia," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.