Pata taarifa kuu

Guatemala:Rais mteule Bernardo Arevalo, asimamisha ushiriki wake katika mabadiliko ya serikali.

Nairobi – Rais mteule wa Guatemala Bernardo Arevalo amesitisha kwa muda ushiriki wake katika kipindi cha mpito cha serikali, alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Rais mteule Bernardo Arévalo akitoa hotuba yaka katika  mkutano na waandishi wa habari katika Jiji la Guatemala, Ijumaa, Septemba 1, 2023.
Rais mteule Bernardo Arévalo akitoa hotuba yaka katika mkutano na waandishi wa habari katika Jiji la Guatemala, Ijumaa, Septemba 1, 2023. AP - Moises Castillo
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lilikuja baada ya ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu kuvamia vituo vinavyosimamiwa na mahakama kuu ya uchaguzi ya Guatemala siku ya Jumanne.

Arevalo ameutaja uchunguzi wa mwendesha mashtaka kuhusu ushindi wake katika uchaguzi kuwa ni sehemu ya jaribio la mapinduzi, na kuelezea uvamizi wa Jumanne kama "uhalifu wa wazi wa matumizi mabaya ya mamlaka kwa madhumuni ya uchaguzi" ambao ulikiuka katiba ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake, serikali ya Rais Alejandro Giammattei ilisema inaheshimu uamuzi wa Arevalo lakini haikubaliani nao kwa sababu ulifanywa kutokana na hatua zaidi ya tawi la mtendaji, "ambazo haziingiliani na mchakato ambao umeendelezwa hadi sasa."

"Tunasisitiza nia yetu thabiti ya kurejesha mara moja mchakato wa mpito mara tu mamlaka iliyochaguliwa itakapoomba," serikali iliongeza.

Arevalo, ambaye alifanya kampeni kwa ahadi za kukabiliana na ufisadi, alishinda kwa kishindo uchaguzi wa awamu ya pili wa Agosti 20.

Waendesha mashtaka walikuwa wametishia kukizuia chama chake, Semilla, kushiriki katika uchaguzi huo, na kusababisha malalamiko ya kimataifa.

Muda mfupi kabla ya maafisa wa mahakama ya uchaguzi kutangaza Arevalo mshindi, chama chake Semilla kiliarifiwa kwamba tawi la mahakama hiyo lilisimamisha chama kwa makosa ya usajili.

Mahakama hiyo imebatilisha kwa muda agizo la kusimamishwa kazi hadi Oktoba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.