Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Bolivia: Polisi yamsaka mtuhumiwa wa mauaji ya mwendesha mashtaka Pecci

Bolivia imezindua operesheni kubwa ya polisi kujaribu kumkamata raia wa Uruguay Sebastian Marset, mfanyabiashara wa dawa za kulevya, anayesakwa nchini mwake, Paraguay na Brazil, na pia na polisi ya Interpol na shirika la Marekani la kupambana na dawa za kulevya.

Maafisa wa polisi ya Bolivia wakiegesha gari mbele ya lango la nyumba iliyopekuliwa kama sehemu ya ukaguzi dhidi ya mhalifu Sebastian Marset, Julai 30, 2023.
Maafisa wa polisi ya Bolivia wakiegesha gari mbele ya lango la nyumba iliyopekuliwa kama sehemu ya ukaguzi dhidi ya mhalifu Sebastian Marset, Julai 30, 2023. AFP - RICARDO MONTERO
Matangazo ya kibiashara

Jina lake linahusishwa na mauaji ya mwendesha mashtaka anayehusika na kupambana na madawa ya kulevya na biashara haramu nchini Paraguay Marcelo Pecci, mnamo mwezi wa Mei 2022, kama mmoja wa waanzilishi wa uhalifu huo.

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Bolivia, Eduardo del Castillo, tangu Jumamosi "msururu wa upekuzi" umefanyika katika kaunti ya Santa Cruz, mashariki mwa nchi na kwenye mpaka wa Brazil na Paraguay, kama sehemu ya msako dhidi ya Sebastian Marset, "mfanyabiashara wa madawa ya thamani ya juu".

"Mtu huyu anatafutwa na polisi ya Interpol, taasisi ya kupambana na dawa za kulevya (Drug Enforcement Administration), na nchi katika eneo hilo, kama vile Uruguay, Brazili na Paraguay," waziri wa mambo ya ndani ameongeza. Tulikusanya askari polisi zaidi ya 2,250, magari zaidi ya 144, tulifanya operesheni zaidi ya 23, misako sita na kukamata watu 12. "Sebastian Marset Cabrera, "mwenye uraia  mwingi", "bado" iko katika kaunti ya Santa Cruz, pamoja na mke wake , raia wa Peru, na watoto wao watatu, amesema.

Kulingana na uchunguzi wa kwanza, mshukiwa huyo aliingia Bolivia mwezi Septemba mwaka jana ambapo aliendeleza baadhi ya shughuli za kijamii, akionekana hasa kama mmiliki wa klabu ya soka ya daraja la pili katika eneo hilo.

Ndugu wawili wa Colombia, ambao walipanga mauaji hayo na kulipa fidia kwa mshambuliaji aliyempiga risasi na kumuua Mwendesha Mashtaka Pecci kwenye ufuo wa bahari nchini Colombia mwaka 2022, walihukumiwa mwezi Mei mwaka jana nchini Colombia kifungo cha miaka 25 na miezi sita jela, kulingana na waendesha mashtaka wa Colombia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.