Pata taarifa kuu
AFYA-HAKI

UN yalaani 'ubaguzi wa rangi ulioenea' dhidi ya wanawake weusi wajawazito Amerika

Wanawake weusi wajawazito katika bara la Amerika wanateswa vibaya kutokana na "ubaguzi wa rangi ulioenea" katika mfumo wa huduma za afya, ambao unawajibika hasa kwa hatari kubwa zaidi ya kufa wakati wa kujifungua, hasa nchini Marekani, unashutumu Umoja wa Mataifakatika ripoti iliyotolewa siku ya Jumatano.

Wanawake weusi waandamana Washington.
Wanawake weusi waandamana Washington. Anne Corpet / RFI
Matangazo ya kibiashara

Vifo wakati wa kujifungua miongoni mwa wanawake wenye asili ya Kiafrika "viko juu kwa hali isiyo ya kawaida, ama kwa maneno kamili au kwa kulinganisha" na wanawake wasio wa asili hii, limebaini shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) katika ripoti hii ambayo inapitia data za nchi tisa za Amerika zilizochaguliwa kwa sababu ya idadi ya wanawake hawa kwa raia na data zinazopatikana (Brazili, Colombia, Costa Rica, Cuba, Panama, Suriname, Trinidad na Tobago, Marekani na Uruguay).

Tofauti hiyo ni kubwa zaidi nchini Marekani, ambako wanawake wenye asili ya Kiafrika wana uwezekano wa kufa mara tatu zaidi ya wanawake wazungu wakati wa ujauzito au ndani ya wiki sita baada ya kujifungua. Na vifo hivi vya uzazi "vinaendelea bila kujali kipato au kiwango cha elimu", inasisitiza ripoti hiyo.

Wanawake weusi pia wana uwezekano wa mara 2.5 zaidi wa kufa wakati wa kujifungua nchini Suriname na mara 1.6 zaidi nchini Brazil na Colombia.

Ikibainisha kuwa vifo hivi vya juu vya uzazi miongoni mwa wanawake weusi katika bara la Amerika mara nyingi huchangiwa na "kushindwa kwao kutafuta matunzo kwa wakati, kwa mtindo wa maisha wenye kutiliwa shaka au mielekeo ya kurithi", UNFPA "inakanusha kimsingi dhana hizi potofu", ikihusisha tofauti hizi na "ubaguzi wa rangi kwa ujumla na ubaguzi wa kijinsia”.

"Janga la ubaguzi wa rangi kwa wanawake na wasichana weusi, ambao wengi wao ni wazao wa waathiriwa wa utumwa, linaendelea katika Amerika", anakashifu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa Natalia Kanem katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Mara nyingi, wanawake na wasichana wenye asili ya Kiafrika wananyanyaswa, mahitaji yao hayachukuliwi kwa uzito na familia zao zinasambaratishwa na vifo vinavyoweza kuzuilika wakati wa kujifungua," anaongeza.

Wanawake weusi na wasichana wanaobalehe kwa ujumla wanakosa fursa “kabla, wakati na baada ya ujauzito,” ripoti hiyo inabainisha. UNFPA inaangazia hasa chuki ambazo zinaendelea katika maudhui ya elimu ya matibabu.

Kwa hivyo, wanawake weusi walio katika leba wananyimwa ganzi kwa kisingizio kwamba watakuwa hawajali sana uchungu au dawa ya kutuliza maumivu kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kuwa tegemezi, inashutumu ripoti hiyo. Pia inakosoa tabia za unyanyasaji wa matusi au kimwili kwa wahudumu wa afya.

Matokeo ya uzembe ambao wao ni waathirika, wanawake hawa wanakabiliwa na matatizo zaidi wakati wa ujauzito wao na huduma iliyoahirishwa, "ambayo mara nyingi husababisha kifo".

Shirika hilo pia linasikitika kutokuwepo kwa data za rangi katika baadhi ya nchi, jambo ambalo linafanya tofauti hizi kuwa "zisizoonekana".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.