Pata taarifa kuu

Marekani: Makamu wa rais wa zamani Mike Pence adhihirisha nia yake ya kugombea uchaguzi

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Mike Pence amewasilisha fomu yake ya kugombea uchaguzi kwenye Ikulu ya Marekani ya White House siku ya Jumatatu, kulingana na nyaraka zilizotolewa na Tume ya Shirikisho ya Uchaguzi (FEC). Mhafidhina huyu wa kiinjilisti atajitenga na Rais wa zamani Donald Trump, ambaye alikuwa makamu wa rais mwaminifu kwake kwa miaka minne, wakati wa kura za mchujo za chama cha Republican wa 2024.

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani na Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence, akiambatana na mkewe Karen Pence, wakizungumza katika hafla iliyofanyika Des Moines, Iowa Juni 3, 2023.
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani na Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence, akiambatana na mkewe Karen Pence, wakizungumza katika hafla iliyofanyika Des Moines, Iowa Juni 3, 2023. © Dave Kaup / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mike Pence atarasimisha Jumatano, Juni 7, siku ya kuzaliwa kwake 64, kuingia kwake katika kinyang'anyiro hiki kwa video, kisha mkutano huko Des Moines, Iowa, mojawapo ya majimbo ya kwanza kupiga kura katika kura ya mchujo. Kisha atahitimisha siku hiyo kwa makala maalumu kwenye kituo cha CNN, kulingana na washirika wake wa karibu.

Anajiunga na uwanja ambao tayari umejaa wagombea wa chama cha Republican, na wagombea kadhaa ambao, kwa wakati huu, rais wa zamani anaonekana kuwapiku kwa kura nyingi kulingana na uchunguzi.

Mike Pence, Mkristo wa Kiinjilisti na ambaye ni mpinzani mkali dhidi ya uavyaji mimba,  alimsaidia Donald Trump kushinda haki ya kidini kama mgombea mwenza wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais 2016. Baada ya miaka kadhaa ya uaminifu usioyumba, sintofahamu kati ya wawili hawa ilishuhudiwa wakati Mike Pence alikataa kumuunga mkono Donald Trump katika kulaani matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2020, uliopelekea ushindi wa Joe Biden kutoka chama cha Democratic.

Sintofahamu kati ya Mike Pence na Donald Trump ilirasimishwa wakati wa shambulio la Capitol

Gavana huyo wa zamani wa Indiana alijitenga na rais wa zamani wa Marekani Donald trump, akimlaumu kwa kumweka katika hatari ya kibinafsi kwa kushangilia washambuliaji wa makao makuu y Bunge Capitol mnamo Januari 6, 2021 alipokuwa na familia yake katika jengo la Congress. Siku hiyo, Mike Pence aliongoza, kama makamu wa rais, kikao cha Congress, ambapo wabunge walitakiwa kuidhinisha ushindi wa Joe Biden. Donald Trump alisisitiza ili aweze kukataa kuidhinisha uchaguzi wa Joe Biden, wakati Mike Pence alikuwa na jukumu tu la kiitifaki.

Gavana huyo wa zamani wa Indiana hakufuata sheria hiyo, jambo ambalo lilimletea uadui mkubwa miongoni mwa wafuasi wa bilionea huyo. Washambuliaji hao walipoingia Capitol kwa nguvu, baadhi walitoa wito wa Mike Pence "kunyongwa" , ambapo ilimbidi kujificha kwa haraka.

Tangu wakati huo alibaini kwamba maneno ya rais yalikuwa "ya kutowajibika" na "yalimtia hatarini". Mike Pence alitangaza huko Gridiron Dinner, wakati wa sherehe iliyoandaliwa na waandishi wa habari kwa watu mashuhuri wa kisiasa, kwamba historia itamfanya Donald Trump "awajibike".

Uhasama huu kati ya wawili hao unahatarisha uwezekano wa Mike Pence, ambaye wanaharakati wengi watiifu kwa Donald Trump wanaendelea kumchukulia kama "mhaini". 

(Pamoja na AFP na Reuters)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.