Pata taarifa kuu

Marekani: Mike Pence amehojiwa kuhusu uvamizi wa majengo ya bunge

NAIROBI – Nchini Marekani, aliyekuwa Makamu wa rais Mike Pence amehojiwa na kamati inayochunguza mchango wa rais wa zamani Donald Trump, kutaka kubadilishwa kwa matokeo ya urais wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020 na kuzua fujo katika majengo ya bunge jijini Washington DC.

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na Mike Pence aliyekuwa naibu wake
Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na Mike Pence aliyekuwa naibu wake AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Pence alihojiwa na kueleza alichokifahamu mbele ya Kamati hiyo kwa zaidi ya saa saba, kwa mujibu wa ripoti za ndani.

Hatua hii imekuja baada ya Trump kupoteza rufaa, aliyokuwa amewasilisha kutaka aliyekuwa Makamu wake kutotoa ushahidi mbele ya Kamati hiyo maalum.

Mapema mwezi huu, Pence alidokeza kuwa alikuwa tayari kufika mbele ya Kamati hiyo baada ya Mahakama kumtaka kufika mbele ya jopo linaloendeleza uchunguzi na kueleza mawasiliano aliyokuwa nayo na Trump kuelekea kuvamiwa kwa majengo ya bunge Januari 6 mwaka 2021.

Pence amefika mbele ya Kamati hiyo, wakati huu akielezwa kuwa huenda akajitokeza  kupambana na Trump kuwania tiketi ya chama cha Republican kuwania urais mwaka 2024. Haikuwekwa wazi ni lini Mike Pence atafika mbele ya jopo hilo.

Kwa miezi kadhaa jopo hilo la mahakama limekuwa likifanya uchunguzi kufuatia tukio la Januari 6 mwaka 2021 , la uvamizi katika jengo la bunge la Marekani na juhudi za Trump na washirika wake kuvuruga matokeo ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.