Pata taarifa kuu

Mmarekani mweusi, aliyezaliwa Kenya auawa mikononi mwa maafisa wa usalama

Maafisa saba wa polisi katika jimbo la Virginia nchini Marekani, wamekamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya daraja la pili dhidi ya Mmarekani mweusi Irvo Otieno.

Mmarekani mweusi Irvo Otieno aliyeuawa mikononi mwa maafisa wa usalama nchini Marekani
Mmarekani mweusi Irvo Otieno aliyeuawa mikononi mwa maafisa wa usalama nchini Marekani © AttorneyCrump
Matangazo ya kibiashara

Otieno mwenye umri wa miaka 28, aliyehamia nchini Marekani na familia yake akitokea Kenya akiwa na umri wa miaka minne, alipoteza maisha, tarehe 6 Machi wakati akihamishwa kutoka gerezani kwenda katika kituo cha afya cha watu wenye matatizo ya akili.

Famila yake inasema, kwa kipindi kirefu, amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili.

Wahudumu watatu pia wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kuhusu mauaji hayo, yaliyofananishwa na yale ya Mmarekani mwingine George Floyd, mwaka 2020.

Mama yake Otieno, Caroline Ouko anahoji ni kwanini mtoto wake aliuawa pamoja na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa akili.

“Kwanini wamemuua mwanangu ? Wamemuua kama mbwa,” amesema baada ya kutazama mkanda wa video wa dakika 12 ulionesha namna Otieno alivyouawa.

 

Uchunguzi wa awali wa kiafya unaonesha kuwa, alipoteza maisha baada ya kukosa hewa, baada ya kupigwa na kuzuiwa chini na maafisa hao wa usalama.

Otieno alikamatwa na kupelekwa  kizuizini Machi 3, kwa madai ya wizi katika mtaa anaoishi wa Richmond.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.