Pata taarifa kuu

DRC: Marekani, mojawapo ya nchi chache zilizoitaka Rwanda kushawishi M23

Mwishoni mwa mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika, Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, aliiomba Kigali mnamo Desemba 15 kuchukua hatua ili kuruhusu kutumika kwa makubaliano ya Luanda na hivyo kundi la M23 kujiondoa kwenye maeneo inayoshikilia.

Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza wakati Rais wa Senegal na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall akitazama wakati wa chakula cha jioni kwa Viongozi wa Marekani na Afrika katika Ukumbi wa Mashariki wa Ikulu ya Marekani mjini Washington, Marekani, Desemba 14, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza wakati Rais wa Senegal na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall akitazama wakati wa chakula cha jioni kwa Viongozi wa Marekani na Afrika katika Ukumbi wa Mashariki wa Ikulu ya Marekani mjini Washington, Marekani, Desemba 14, 2022. REUTERS - ELIZABETH FRANTZ
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine tena, Marekani inaweka shinikizo kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusiana na mzozo wa usalama unaohusishwa na waasi wa M23. Hata hivyo, Marekani imetengwa katika suala hili kimataifa, kama anaelezea Jason Stearns, mkurugenzi wa kundi la Utafiti kwa DRC, kituo cha utafiti kinachounganishwa na Chuo Kikuu cha New York.

"Kwa miezi michache iliyopita ambapo Marekani imekuwa ikipaza sauti yake kuitaka Rwanda kusitisha uungaji mkono wake kwa M23, wakati huu Antony Blinken alikuwa mpole zaidi. Hata hivyo, katika taarifa nyingine, wajumbe wa Bunge la Marekani na hata watendaji wakuu wa Marekani wamekuwa wazi na wenye nguvu katika kulaani uungaji mkono wa Rwanda. Kwa hivyo nadhani ni nyongeza ya sera ambayo tayari ilikuwepo na ambayo Marekani iko peke yake kidiplomasia. Kwa kawaida Marekani huendeleza sera yake na washirika wanaopendelea, hasa ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa - Ufaransa na Uingereza - na ni nchi hizi mbili, Ufaransa na Uingereza, ambazo zinazuia kwa sababu, nadhani, kwa sababu ya masilahi yao wenyewe katika kanda. Nchi hizi mbili kwa hiyo zimesitasita hata kama, kwa faragha, wanadiplomasia wa nchi hizi mbili wanatambua kuwa msaada huu upo”, amebainisha.

Wakati wa mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika, Paul Kagame hakukutana na Anthony Blinken, tofauti na Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi. Rais wa Rwanda hakushiriki katika picha ya mwisho ya mkutano karibu na Joe Biden. Kwa nini tofauti hii? Jason Stearns, anatupa baadhi ya majibu.

"Nadhani ni juu ya kuonyesha umuhimu wa DRC kwa Marekani. Sio tu kwa sababu ya ukubwa wa nchi na maadili ya kidemokrasia, nk ... lakini pia ni kwa sababu ya siasa za kijiografia. Kongo ndio mzalishaji mkubwa wa kobalti ulimwenguni na mzalishaji mkubwa wa shaba barani Afrika. Pia kuna akiba kubwa ya lithiamu na madini mengine nchini DRC. Nadhani hiyo ni sehemu ya umuhimu wa DRC na ndiyo maana walikutana. Ndivyo ilivyo, nadhani kwa serikali hii ya Biden, angalau, kuna wanachama ambao wanasisitiza sana maadili ya demokrasia. Umuhimu wa Rwanda, kama mshirika katika kanda, umepungua sana, kwa miaka michache sasa. Sio tu chini ya Biden. Nadhani haya ndiyo mambo yanayoelezea dhamira hii baada ya Tshisekedi na ukosefu huu wa umuhimu kwa kukutana na Kagame, "anachambua Jason Stearns, mkurugenzi wa kundi la Utafiti kwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.