Pata taarifa kuu

Miaka hamsini baada ya ujumbe wa mwisho wa Apollo, Marekani inarejea Mwezini

Huko Cape Canaveral, Florida, NASA imeanzisha mchakato wa kuelekea mwezini. Roketi kubwa ya kwanza ya programu ya Artemis imeratibiwa kupaa Jumatatu asubuhi karibu 8:33  saa za Marekani. 

Zoezi la kuelekea Mwezini litakalo zinduzi katika kituo cha safari za mbali cha Kennedy, Agosti 28, 2022.
Zoezi la kuelekea Mwezini litakalo zinduzi katika kituo cha safari za mbali cha Kennedy, Agosti 28, 2022. AP - John Raoux
Matangazo ya kibiashara

Safari hii ya kwanza ya ndege ya majaribio haitakuwa na mtu, lakini lengo la Marekani ni kuwatuma wanaanga kurudi Mwezini mnamo 2025 na kubaki huko.

Mvua ilikuwa inanyesha kwa saa chache zilizopita. Ikiwa hii itaendelea, itazuia kupaa kwa chombo hiki na uzinduzi utalazimika kuahirishwa hadi Septemba 2. Wakati huohuo, kando ya barabara, mamia ya maelfu ya Waamarekani wamekusanyika wakiwa katika mahema na magari yao, huku wakiwa wamefungasha vyakula, ili wasikose kujionea kwa macho yao safari hii kuelekea Mwezini.

Kwa sababu miaka 50 baada ya ujumbe Apollo, matamanio sio tu kutembea kwenye Mwezi, lakini kubaki huko. "Lazima ufikirie Mwezi kama bara jingine la Dunia," anasema Philippe Berthe, mhandishi kutoka Ufaransa. Wazo ni kupanua uwanja wa shughuli za kibinadamu, ambazo hadi sasa zimezuiliwa kwenye uso wa Dunia bila shaka, lakini pia kwa mzunguko wa chini, kwa Mwezi, kuwa na watu ambao wataishi ama kuzunguka Mwezi."

SLS ni gari lenye nguvu zaidi la mwezini kuwahi kutengenezwa na Nasa, na itakuwa msingi NASA wa mradi  wa  Artemis unaolenga kuwarejesha watu tena katika sakafu ya mwezi baada ya  miaka 50 bila mtu yeyote kwenda huko. 

Kazi yake itakuwa ni kusukuma kifaa cha kuchukua vipimo (pad), kinachoitwa  Orion, mbali na dunia.

Chombo hiki cha anga za mbali kitauzunguka mwezi kabla ya kurejea  duniani kwa kasi kubwa itakayopelekea chombo hicho kupasuka ndani ya Bahari ya Pacific katika kipindi cha wiki sita. 

Orion kinasafiri anga za mbali bila mhudunu yeyote ndani yake na watengenezaji wake wanafikiri kuwa iwapo kitaweza kufanya kazi kama kinavyotarajiwa basi wataalamu wa anga za mbali wataweza kupanda ndani yake kwa ajili ya msururu wa safari ngumu zaidi, wanazotarajia kuanza katika mwaka  2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.