Pata taarifa kuu

Brazil: Maelfu ya watu asili wa Brazil waandamana dhidi ya Jair Bolsonaro

Wakiwa wamevalia mavazi yao ya kitamaduni, maelfu ya watu asili waliandamana na kukusanyika kwenye eneo moja kubwa kilomita nne kutoka ikulu ya rais, makao makuu ya Baraza la Wawakilishi na Mahakama ya Juu zaidi huko Brasilia. Tukio hili linatokea miezi sita kabla ya uchaguzi wa urais, na walikuja kushutumu ufisadi unaodidimiza kiuchumi wa maeneo yao.

Watu asili wa Xikrin huko Brasilia, Brazili, Jumatatu, Aprili 4, 2022.
Watu asili wa Xikrin huko Brasilia, Brazili, Jumatatu, Aprili 4, 2022. AP - Eraldo Peres
Matangazo ya kibiashara

"Tmekuja hapa kuomba serikali ya shirikisho kukomesha vitisho vinavyotanda katika maeneo yetu," Sinezio Trovao, mwakilishi wa kabila la Maguta-Tikuna, mmoja wa kutoja jamii ya watu asili muhimu nchini humo, ameliambia shirika la habari la AFP. Watu asili wapatao 8,000 walikusanyika Brasilia kwa maadhimisho ya kambi ya Terra Livre (ardhi huru), maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka. Yaliandaliwa na ABIP, shirika linalowakilisha watu asili nchini Brazili.

Baada ya miaka miwili ya shughuli kwa njia ya mtandao kutokana na janga la Covid-19, mkutano ulifanyika wakati sheria inayoidhinisha uchimbaji madini katika hifadhi za kiasili inakaribia kupigiwa kura na wabunge wa Brazil. Rais wa sasa Jair Bolsonaro, aliyeingia madarakani mwaka wa 2019, alikuwa ameahidi kufungua hifadhi za kiasili zilizopo, ambazo tayari zimeathiriwa sana na ukataji miti, kwa tasnia ya uchimbaji.

Watu asili waliokusanyika Brasilia kwenye mikutano ya utetezi wa haki zao wanawakilisha 0.2% ya Wabrazili milioni 212, lakini kutoridhishwa kwao kunachukua takriban 13% ya nchi nzima. Ujumbe wao mkuu: "Brazili ni yetu, sio ya Bolsonaro, wala ya wanasiasa wafisadi". Wote wanalaani uharakishwaji wa miradi ya kiuchumi katika maeneo yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.