Pata taarifa kuu

Brazili: Mafuriko makubwa yaripotiwa katika jimbo la Bahia, maji na umeme vyakatwa

Jimbo la Bahia limekumbwa na mvua kubwa tangu mwezi Novemba. Siku ya Ijumaa, Desemba 24, Dhoruba ya kitropiki ilisababisha manispaa 66 kuwekwa cini ya  hali ya dharura. Mashirika ya kutoa misaada yameanza kutoa misaada, lakini hali inaendelea kuwa ngumu.

Mafuriko huko Itamaraju, kusini mwa jimbo la Bahia nchini Brazili, Desemba 2021.
Mafuriko huko Itamaraju, kusini mwa jimbo la Bahia nchini Brazili, Desemba 2021. Isac NOBREGA Brazilian Presidency/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Nyumba, masoko, barabara na madaraja: katika sehemu moja ya Jimbo la Bahia, vyote vimesombwa na maji. Tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba, mvua kubwa inaendelea kunyesha katika eneo hili la Brazil, na kusababisha vifo vya watu 17.

Lakini wikendi hii ya Krismasi, dhoruba ya kitropiki ilipiga eneo hilo. Katika jiji la Salvador, mji mkuu wa jimbo la Bahia, mvua kubwa ilinyesha Ijumaa pekee, mara tano ya wastani wa mwezi mzima wa Desemba.

Manispaa 66 sasa "ziko katika hali ya dharura kabisa", ametangaza gavana wa Bahia. Serikali ya shirikisho na majimbo jirani yanatuma helikopta, boti na wafanyakazi kwenye eneo la tukio ili kuwahamisha wakaazi walio katika dhiki.

Malazi ya muda yamepangwa kwa wale ambao wamepoteza kila kitu. Gridi ya umeme imeharibiwa, na hakuna tena maji ya kunywa.

Lakini shughuli za usaidizi zinaonekana kuwa ngumu. Na wataalamu wa hali ya hewa wanatabiri mvua kubwa zaidi Jumapili hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.