Pata taarifa kuu
BRAZIL-HAKI

Kifo cha kikatili cha mkimbizi wa Kongo chazua ghadhabu nchini Brazil

Katika mji mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro, Moïse Kabagambe, kijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye alikuwa amekimbilia Brazili tangu utotoni, alipigwa hadi kufa baada ya kwenda kudai mshahara wake, kulinana na vyanzo vya usalama nchini humo.

Mnamo Januari 24, Moïse Kabagambe alikwenda kuchukua mshahara wake kwa siku mbili za kazi ambazo alikuwa hajalipwa alipokuwa akifanyia kazi kwenye ufuo wa Tijuca, familia yake imesema.
Mnamo Januari 24, Moïse Kabagambe alikwenda kuchukua mshahara wake kwa siku mbili za kazi ambazo alikuwa hajalipwa alipokuwa akifanyia kazi kwenye ufuo wa Tijuca, familia yake imesema. © AP/Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Januari 24, Moïse Kabagambe alikwenda kuchukua mshahara wake kwa siku mbili za kazi ambazo alikuwa hajalipwa alipokuwa akifanyia kazi kwenye ufuo wa Tijuca, familia yake imesema. Alipoanza kudai mshahara wake, wanaume kadhaa akiwemo muajiri wake walimpiga kwa fimbo, mateke na ngumi.

Tukio hilo lililorekodiwa lilirushwa na polisi. Baada ya dakika kumi na tano za kupigwa, kijana huyo alipoteza fahamu. Mmoja wa washambuliaji wake basi alijaribu kumsaidia, bila mafanikio.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, washambuliaji wawili walijiwasalimisha kwa polisi, na kukiri kuhusika na mauaji hayo, lakini wakikanusha nia yao ya kumuua kijana huyo.

Katika mitandao ya kijamii, mmoja wa washtakiwa alikana ubaguzi wowote wa rangi katika tukio hilo. Kama machafuko hutokea kila siku nchini Brazili, ghadhabu inayosababishwa na tukio hili, ambayo huenda ilitokana na ubaguzi wa rangi, ni kubwa, hasa katika jamii za watu weusi kutoka DRC.

Ili kudhihirisha hasira zao maandamano makubwa yamepangwa kufanyika Jumamosi, Februari 5. Kwa upande wao, ubalozi wa DRC na vyama vya haki za binadamu vinafuatilia kesi hiyo kwa karibu.

"Sisi si wezi wala si wauaji. Na mnawezaje kumuua ndugu yangu aliyekuwa akifanya kazi? Haki!", alisema kaka yake Moïse Kabagambe wakati wa mazishi.

Akihojiwa na wanahabari wa eneo hilo, mama wa mwathiriwa alibaini kwamba familia yake iliondoka DRC kwa kuhofiausalama wao kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo. Kati ya washambuliaji watano, watatu walikamatwa na polisi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.