Pata taarifa kuu

Joe Biden: Tuko tayari kudhibiti kirusi cha Omicron

Wakati idadi ya kesi za Covid-19 inaongezeka kwa kasi na kirusi kipya cha Omicron hatimaye kikitawala nchini Marekani, rais wa nchi hiyo Joe Biden aliwahakikishia raia wake Jumanne, Desemba 21 na kutangaza njia mpya za vipimo, chanjo na mfumo wa hospitali. Rais wa Marekani pia amewaonya wale ambao bado hawajachanjwa, mara nyingi kwa sababu za kisiasa.

Rais wa Marekani Joe Biden akilihutubia taifa Ikulu ya White House mjini Washington, Desemba 21, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden akilihutubia taifa Ikulu ya White House mjini Washington, Desemba 21, 2021. © AP - Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Chanjo ni "wajibu wa kizalendo". Mbali na kutangaza njia za kijeshi kusaidia mfumo wa hospitali na mahitaji ya uzalishaji kwa vipimo vya kibinafsi milioni 500, Joe Biden alizungumzia moja kwa moja Jumanne kuhusiana na Marekani nyingine, ambayo inapinga uhalali wake, akimaanisha Wamarekabi ambao bado wanachukuliachanjo hiyo kwa misingi ya kisiasa, akinyooshea kidole cha lawama wafuasi wa Donald Trump.

"Nilipata dozi yangu ya tatu haraka iwezekanavyo na siku moja tu baadae rais wa zamani alipokea chanjo yake. Hili linaweza kuwa mojawapo ya mambo machache ambayo yeye na mimi tunakubaliana. Wale walio na kumbukumbu zao wanalindwa sana. Jiunge nao, jiunge nasi. "

Joe Biden ameenda mbali zaidi kwa kumpongeza mtangulizi wake kwa kuanzisha utafiti wa chanjo: "Shukrani kwa utawala uliopita na kwa jumuiya yetu ya wanasayansi, Marekani ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza kuwa na chanjo. "

Lakini upinzani ni wa kusuasua. Warepublican wengi wamechukua hatua za kisheria dhidi ya hitaji la chanjo kwa kampuni kubwa. "Ninajua kuwa chanjo za lazima sio maarufu, lakini niliagiza ziwekwe, lakini sio kudhibiti maisha yenu, lakini kuyaokoa na kuokoa ya wengine," Joe Biden alisema.

" Tuko tayari "

Wakati wa hotuba yake kwa njia ya televisheni, Rais wa wa Marekani alizungumza kwa kirefu kuhusu aina mpya ya kirusi cha Omicron, ambacho kimewaambukiza raia wengi nchini Marekani (73.2% ya maambukizi mapya wiki iliyopita). "Lazima sote tuwe na wasiwasi kuhusu Omicron" lakini "tusiwe na hofu," Joe Biden alisema, na kuongeza kuwa nchi "haipo tena katika mwezi wa Machi 2020", wakati Covid-19 ilizuka nchini Marekani na kusababisha vifo na kuzua hofu mongoni mwa raia. "Tuko tayari," amewahakikishia raia wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.