Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA

Mexico: Wahamiaji 53 wafariki katika ajali ya barabarani karibu na Guatemala

Takriban wahamiaji 53, wengi wao kutoka Guatemala, walifariki katika ajali ya lori iliyotokea katika eneo la Chiapas, kusini mwa Mexico, siku ya Alhamisi.

Miili ya wahamiaji waliofariki katika ajali ya barabarani imepangwa kwenye barabara ya Tuxtla Gutierrez, katika jimbo la Chiapas nchini Mexico.
Miili ya wahamiaji waliofariki katika ajali ya barabarani imepangwa kwenye barabara ya Tuxtla Gutierrez, katika jimbo la Chiapas nchini Mexico. SERGIO HERNANDEZ AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hao walijazwa kwenye lori, kulingana na maelezo ya awali kwa vyombo vya habari vya kiosi cha Ulinzi wa Raia. Dereva anadaiwa kutorojka baada ya kupoteza udhibiti wa gari lake lililopinduka, vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti.

Lori hilo liliripotiwa kuendeshwa kwa kasi kabla ya kupoteza mwelekeo katika kona na kugonga daraja la raia katika barabara kuu inayoelekea katika mji mkuu wa jimbo la Chiapas, Tuxtla Gutierrez.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alielezea ajali hiyo kuwa ya uchungu na kuandika katika twitter kwamba 'anajutia ajali hiyo'.

Takriban watu 100, wanaodaiwa kuwa wahamiaji kutoka Marekani ya kati walikuwa ndani ya lori hilo wakati lilipopindukia na kugonga daraja katika jimbo la Chiapas.

Mpaka wa Marekani na Mexico ni mojawapo ya mipaka hatari zaidi duniani kulingana na data kutoka kwa shirika la wahamiaji duniani IOM.

Mwaka huu pekee takriban watu 650 wamefariki katika mpaka huo, wakijaribu kuvuka, ikiwa ni zaidi ya mwaka wowote ule tangu IOM ilipoanza kuweka rekodi zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.