Pata taarifa kuu

Marekani yakabiliwa na wimbi la mgomo

Maelfu ya wafanyakazi nchini Marekani wanaendelea na mgomo katika maeneo mengi ya nchi hiyo. Wanalaani mazingira magumu ya kazi wakati waajiri wao wanpata faida kubwa.

Wafanya kazi wa kampuni kubwa ya mashine za kilimo John Deere wakiwa katika mgomo huko Davenport, Iowa, Marekani, Oktoba 15, 2021.
Wafanya kazi wa kampuni kubwa ya mashine za kilimo John Deere wakiwa katika mgomo huko Davenport, Iowa, Marekani, Oktoba 15, 2021. Getty Images via AFP - SCOTT OLSON
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya raia nchini Marekani tayari wameuita mwezi wa Oktoba kama "Striketober" kwa sababu ya kuongezeka kwa migomo kote Mnchini Marekani. Wafanya kazi kutoka viwanda vya nafaka, viwanda vinavyotengeneza matrekta, shule, au hata hospitali, wote kwa pamoja ni maelfu ya wafanyikazi wanaogoma au wanaotishia kugoma.

Wafanyakazi 10,000 kutoka kiwanda kinachotengeneza matrekta cha John Deere wanagoma tangu Alhamisi wiki iliyopita;  Wafanyakazi 1,400 katika kiwanda cha nafaka cha Kellogg wanagoma tangu Oktoba 5, na zaidi ya wafanyakazi 2,000 katika Hospitali ya Mercy huko Buffalo wanagoma tangu Oktoba 1. Wafanyakazi wengine 31,000 wa kituo cha afya cha Kaiser Permanente magharibi mwa Marekani wanatishia kuanzisha mgomo hivi karibuni.

Wengi wanalaani mazingira magumu ya kazi na wanaandamana dhidi ya mabadiliko katika mikataba ya kijamii. Kampuni nyingi zinataka kuondoa marekebisho ya moja kwa moja ya mshahara kwa gharama ya maisha, wakati mfumuko wa bei ni mkubwa. Vyama vya wafanyakazi na wafanyikazi wameghadhabishwa zaidi kwani waajiri wao walipata mauzo makubwa wakati wa mgogoro wa kiafya uliosababishwa na COVID-19 wakati walipolazimika kufanya kazi ngumu zaidi kuhakikisha kazi hazisimami.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.