Pata taarifa kuu

Wataalam watatu wa Marekani watunukiwa Tuzo ya Nobel ya uchumi

Tuzo ya Nobel katika uchumi imetolewa Jumatatu hii Oktoba 11 kwa wataalam watatu wa uchumi waliobobea, wote wakiwa wanaishi nchini Marekani.

Tangazo la Tuzo ya Nobel ya Uchumi, katika Chuo cha Sayansi cha Royal Sweden huko Stockholm, Oktoba 11, 2021.
Tangazo la Tuzo ya Nobel ya Uchumi, katika Chuo cha Sayansi cha Royal Sweden huko Stockholm, Oktoba 11, 2021. AFP - CLAUDIO BRESCIANI
Matangazo ya kibiashara

Washindi hao ni David Card kutoka Canada, wa Chuo Kikuu cha California huko Berkeley, ambaye alipokea nusu ya thamani ya tuzo hiyo; nusu nyingine amepokeaJoshua Angrist wa Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts na Guido Imbens wa Chuo Kikuu cha Stanford huko California.

Kulingana na majaji, washindi hawa watatu "walibadilisha kabisa kazi ya ufundi katika sayansi ya uchumi".

"Utafiti wao umeboresha sana uwezo wetu wa kujibu maswali muhimu, ambayo yamekuwa na faida kubwa kwa jamii," ameongeza Peter Fredriksson, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi katika Royal Swedish Academy.

Tofauti na zawadi zingine za Nobel, tuzo ya uchumi haikuanzishwa na wosia wa Alfred Nobel. Badala yake, Benki Kuu ya Sweden ilifanya hivyo katika kumbukumbu yake mnamo mwaka 1968, mshindi wa kwanza akichaguliwa mwaka mmoja baadaye. Hii ndio tuzo ya mwisho kutangazwa kila mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.