Pata taarifa kuu
MAREKANI

Septemba 11, ukurasa wa historia kwa vijana waliozaliwa baada ya 2001

Kila mtu anajua kilichotokea Septemba 11, 2001, siku ya mashambulio mabaya zaidi ya kigaidi katika historia ya Marekani. Isipokuwa kizazi kilichozaliwa wakati au baada ya tukio hilo ambalo liligharimu maisha ya karibu watu 3,000. Kwa hivyo ni muhimu kwa vijana wa leo kufahamu kilichotokea Septemba 11, 2àà& nchini Marekani.

Minara pacha ya Kituo cha Biashara duniani World Trade Center kilichogongwa na ndege zilizotekwa nyara kabla ya kudondoka
Septemba 11, na kusababisha vifo vya karibu watu 3,000.
Minara pacha ya Kituo cha Biashara duniani World Trade Center kilichogongwa na ndege zilizotekwa nyara kabla ya kudondoka Septemba 11, na kusababisha vifo vya karibu watu 3,000. AFP - HENNY RAY ABRAMS
Matangazo ya kibiashara

Ni miaka 20 tangu kutokea kwa shambulio baya nchini Marekani, shambulio lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Al Qaeda la Osama bin Laden.

Mshtuko wa mashambulio ya Septemba 11, ungeweza kuwa umeshasahaulika hasa kwa watu wenye chini ya umri wa miaka 30 ambao hawana kumbukumbu nzuri ya siku ya tukio. Lakini kwa Wamarekani wengine wanaoishi mbali na miji ya New York ama Washington, matukio yamekuwa sehemu ya historia.

Shambulio la kigaidi la Septemba 11 2001, liliiumiza Marekani moyoni kwa namna tofauti. Shambulio la ukubwa huu halikuwahi kutokea katika ardhi ya nchi hiyo hapo kabla. Siyo tu kwa kuzungumzia idadi ya watu waliokufa ama waliojeruhiwa. Lakini pia usahihi wa namna magaidi walivyoangamiza alama za uwezo wa kiuchumi na kijeshi wa nchi hiyo duniani, ndani ya saa moja.

Hadi hii leo, hakujawahi kutokea shambulio linalokaribia kiwango cha shambulizi la 9/11.

Septemba 2001, ulikuwa ni mwaka wa kwanza wa George W. Bush madarakani kama Rais wa Marekani. Alipokea pongezi nyingi kwa kutangaza kwamba atamuwinda mhusika mkuu wa shambulio la Septemba 11 yaani Osama bin Laden.

Kile kilichojulikana kama "Vita dhidi ya ugaidi" tangu wakati huo kimesababisha uvamizi wa Afghanistan, kisha Iraq, kuchipuka kwa Isis na kuenea kwa maelfu ya waasi wanaoungwa mkono na Iran kote Mashariki ya Kati, vifo vya maefu ya wanajeshi, wanawake na raia wengi wa kawaida.

Ugaidi haujatokomezwa - kila nchi kuu ya Ulaya imekumbwa na mashambulio katika miaka ya hivi karibuni - lakini kumekuwa na mafanikio pia.

Ijumaa hii, Septemba 10, ili sehemu hii ya historia isijulikane tu lakini pia iendelezwe, wanafunzi 90 wa mwaka wa mwisho wa shule ya upili ya Ufaransa walikusanyika na kukaa kimya kwa dakika moja katika ukumbi mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.