Pata taarifa kuu
MAREKANI-TOVUTI

Marekani yazuia tovuti 33 zinazodhibitiwa na Irani

Idara ya sheria nchini Marekani imefahamisha Washington imeamuru kufungia tovuti 33 za habari zenye kufungamana na utawala wa Teheran  Iran kufuatia kile Marekani inasema tovuti hizo zimekuwa zikipotosha na kueneza habari za uwongo. Kwa mujibu wa serikali ya Marekani, haya ni matokeo ya vikwazo vya serikali ya Joe Biden dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Picha ya skrini ya runinga ya Al-Alam, moja ya tovuti ambayo imezuiwa na idara ya sheria ya Marekani.Juni 23 2021
Picha ya skrini ya runinga ya Al-Alam, moja ya tovuti ambayo imezuiwa na idara ya sheria ya Marekani.Juni 23 2021 © via REUTERS - REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari idara hiyo ya sheria ya Marekani imefahamisha kuwa tovuti hizo zimekuwa zikitumiwa na vyombo vya habari pamoja na runinga inayomilikiwa na serikali ya Teheran kwa kueneza tarifa zisizo za kwelinia ikiwa ni kuwapotosha wapiga kura wa Marekani kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.

Unapojaribu kutembelea tovuti inayofahamika kama Al-Alam, idhaa ya Kiarabu ya sauti ya Iran, au Al-Masirah, pamoja na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kundi la waasi wa Houthi washirika wa Yemen wa Tehran ujumbe unaokuja ni: chaneli hii imefungwa.

Mbali na vyombo hivyo vya habari tovuti zilizounganishwa na vikundi vyenye silaha vya Iraq jirani na Iran zinaonyesha ujumbe huo huo.

Marekani imesema tovuti tatu kati ya hizo 33 zilikuwa zinaendeshwa na kundi la Kata'ib Hizballah, ambalo zaidi ya muongo mmoja uliopita lilitajwa kuwa kundi la kigaidi.

Kundi hilo ni tofauti na lile la wanamgambo wa Hezbollah ambalo tovuti zake za habari zinaendelea kufanya kazi.

Tangazo la Marekani linajiri saa chache tu baada ya shirika la habari la serikali ya Iran IRNA kusema, Marekani ilizifunga tovuti za Iran bila ya kutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.