Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA-UCHUMI

Bunge la Seneti laahirisha mjadala juu ya mpango wa kuinua uchumi wa Biden

Baraza la Senati la Marekani ambalo lilitarajia Alhamisi wiki hii kuanza kujadili mpango wa rais Joe Biden wa kukabiliana na janga la Corona na kuimarisha uchumi utakaogharimu dola trilioni 1.9  limeahirisha kuanza kwa mjadala huo.

Makao makuu ya Bunge la Marekani Capitol Hill huko Washington (picha ya kumbukumbu).
Makao makuu ya Bunge la Marekani Capitol Hill huko Washington (picha ya kumbukumbu). AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kutoka Bunge la Senetri la Marekani mjadala huo utaanza hadi pale nakala kamili ya muswada huo wa kurasa 628 utakaposomwa kwa sauti.

Warepublican wanapinga muswada huo wa sheria ambao wademokrat wanapendekeza pia ugharimie miradi yao muhimu.

Kura juu ya kupitishwa kwa mpango wa rais Joe Biden wa kukabiliana na janga la Corona na kuimarisha uchumi inaweza kufanyika mwishoni mwa wiki. Warepublican, ambao wanaweza kuchelewesha mchakato huo, tayari wameomba nakala ya muswada huo isomwe kwa sauti. Ikiwa itasomwa kwa sauti inaweza kuchukua hadi saa 10.

Wademocrats, ambao hawawezi kutegemea msaada kutoka kwa Warepublican, wamesema wanataka kuongeza marekebisho kwenye muswada huo, wakitoa msaada zaidi kwa majimbo madogo na kulipa pesa zaidi kwa maendeleo ya miundombinu.

Mpango wa kukabiliana na janga la Corona na kuimarisha uchumi wa Joe Biden, ulioitwa American Rescue Plan, ulipitishwa mwezi uliopita na Baraza la Wawakilishi. Utawezesha kufadhili kampeni ya chanjo na ununuzi wa vifaa vya matibabu, na pia hatua mpya za msaada kwa familia, wafanyabiashara wadogo na serikali za mitaa.

Baraza la Seneti la Marekani liliendelea na kikao chake licha ya onyo kutoka kwa polisi wa Capitol Hill huko Washington kwamba walihofia shambulio kama lile la Januari 6 Alhamisi wiki hii, ni waandamanaji wachache tu walioripotiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.