Pata taarifa kuu
MAREKANI- AFYA

Dk Fauci Kuvaa barakoa inaweza kuwa muhimu hadi mwaka 2022 nchini Marekani

Karibu mwaka mmoja uliopita, Marekani ilitangaza kifo cha kwanza kutokana na janga la COVID-19. Leo, ingawa chanjo inaendelea, nchi hiyo bado ni moja ya nchi zilizoathirika zaidi na janga hilo duniani.

Daktari Anthony Fauci mkurugenzi mkuu wa idara ya kitaifa kuhusu magonjwa yanayosababishwa na virusi mbele ya tume ya afya ya Bunge la Congress Marekanile Juni 23 2020.
Daktari Anthony Fauci mkurugenzi mkuu wa idara ya kitaifa kuhusu magonjwa yanayosababishwa na virusi mbele ya tume ya afya ya Bunge la Congress Marekanile Juni 23 2020. POOL / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati mwandishi wa CNN akimuuliza ikiwa Wamarekani bado watavaa barakoa mnamo mwaka 2022, Dk Fauci, mshauri mkuu wa masuala ya matibabu wa Joe Biden kuhusu COVID-19, amesema raia wanatakiwa kuwa wangalifu. Kwa upande wake anasema "Nadhani inawezekana kabisa watu kuendelea kuvaa barakoa hadi mwishoni mwa mwaka 2022".

Mtaalam namba moja wa matibabu kuhusu COVID-19 kwenye timu ya White House anasema kwamba kila kitu kitategemea maendeleo ya chanjo na kupungua kwa maambukizi mapya.

Wakati huo huo Dk Fauci amewataka raia kuendelea kuheshimu hatua za kiafya ili kuepuka maambukizi mapya.

Kwa wiki mbili zilizopita, Marekani ilirekodi kupungua kwa maambukizi mapya na zaidi ya watu milioni moja na nusu hupewa chanjo kila siku. Marekani inakaribia kufikia idadi ya vifo 500,000.

Mkurugenzi huyo wa kituo cha magonjwa ya kuambukiza bado ana matumaini na amehakikisha kuwa ikiwa maambukizi mapya yataendelea kupungua, vizuizi vinaweza kuondolewa hatua kwa hatua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.