Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-BIDEN-SIASA

Marekani 2020: Trump na Biden wasubiriwa Midwest kabla ya uchaguzi Novemba 3

Siku tatu kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, Rais wa nchi hiyo Donald Trump na mpinzani wake kutoka chama cha Democratic Joe Biden watakuwa katika kampeni ya uchaguzi katika majimbo muhimu huko Midwest.

Joe Biden na Donald Trump, wagombea urais katika uchaguzi wa urais wa Marekani.
Joe Biden na Donald Trump, wagombea urais katika uchaguzi wa urais wa Marekani. AP/Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump atasafiri kwenda Michigan, Wisconsin na Minnesota leo Ijumaa, wakati Joe Biden atasafiri kwenda Wisconsin, Minnesota na Iowa.

Michigan na Wisconsin ni majimbo mawili ya kijadi kwa chama cha Democratic ambapo kura zilikaribiana kwa pande mbili wakati wa uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2016 na ambapo Donald Trump kutoka chama cha Republican aliibuka mshindi.

Siku za mwisho za kampeni ziliendelea kutawaliwa na janga la Corona, ambalo limesababisha vifo vya watu 228,000 nchini Marekani na kuharibu uchumi.

Kitengo katika ikulu ya White Haouse kinacho kabiliana na mgogoro wa afya unaosababishwa na Corona kimetangaza kuwa sehemu kubwa ya nchi inakabiliwa na ongezeko la visa vya COVID-19, kwani angalau majimbo tisa yaliripoti kuongezeka kwa visa siku ya Alhamisi, kulingana na takwimu kutoka shirika la habari la REUTERS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.