Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi Marekani: Idadi ya kura kwa njia ya posta yazidi milioni 70

Zaidi ya Wamarekani milioni 70 tayari wamepiga kura kwa njia ya posta katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, sawa na zaidi ya nusu ya jumla ya waliojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2016, wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi, kulingana na takwimu zilizotolewa na U.S. Elections Project.

Uchaguzi wa urais nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba 3.
Uchaguzi wa urais nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba 3. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo, ambayo inaonyesha kasi ya rekodi ambayo inaweza kupelekea idadi kubwa zaidi ya wapiga kura katika zaidi ya karne moja, ni ishara ya hivi karibuni ya nia kubwa katika vita kati ya rais wa kutoka chama cha Republican Donald Trump na mpinzani wake wa kutoka chama cha Democratic Joe Biden.

Pia idadi hiyo inaonyesha hamu ya wapiga kura kupunguza hatari ya kuambukizwa virusi vya Corona wakati kunaripotiwa mlipuko mpya wa janga hilo, huku msimu wa baridi ukikaribia.

Kwa ujumla, chama cha Demokratic kina nafasi karibu mbili kwa moja katika idadi ya kura za mapema. Hata hivyo chama cha Republican kimepunguza pengo kupitia upigaji kura wa mapema kwa mtu katika wiki za hivi karibuni, kama zinavyoonyesha takwimu zilizokusanywa, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.