Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais: Zaidi ya wapiga kura milioni 10 tayari wamepiga kura Marekani

Kura zaidi ya milioni kumi kwa uchaguzi wa urais wa Novemba 3 nchini Marekani tayari zimehesabiwa, idadi kubwa kwa ile ya miaka minne iliyopita na hivyo kuonekana kuwa kiwango cha ushiriki kiko juu zaidi, kulingana na shirika la Elections Project, ambalo hukusanya data kuhusu upigaji kura wa mapema nchini humo.

Kulingana na habari kutoka Chuo Kikuu cha Florida kuhusu majimbo yanayoripoti data za uchaguzi wa mapema, karibu Wamarekani milioni 10.4 tayari wamepiga kura katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Novemba 3.
Kulingana na habari kutoka Chuo Kikuu cha Florida kuhusu majimbo yanayoripoti data za uchaguzi wa mapema, karibu Wamarekani milioni 10.4 tayari wamepiga kura katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Novemba 3. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ongezeko hili linakuja katika hali ambako Marekani inaendelea kukumbwa na mgogogoro wa kiafya unaosababishwa na virusi vya Corona, hali ambayo imesababisha utumiaji mkubwa wa upigaji kura wa mapema na upigaji kura kupitia njia ya posta, hasa kati ya wafuasi wa chama cha Democratic.

Hivi karibuni rais wa Donald Trump, kutoka chama cha Republican, alizua gumzo baada ya kusema kuwa hana imani na mfumo wa uchaguzi kwa njia ya posta, akibaini kwamba itasababisha udanganyifu mkubwa, Lakini mpizabni wake katika uchaguzi huo Joe Bien alisema hizo bi shutuma zisizo kuwa na msingi.

Kulingana na habari kutoka Chuo Kikuu cha Florida kuhusu majimbo yanayoripoti data za uchaguzi wa mapema, karibu Wamarekani milioni 10.4 tayari wamepiga kura katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Novemba 3 kati ya Donald Trump Joe Biden.

Kwa kulinganisha, mnamo Oktoba 16, 2016, wapiga kura milioni 1.4 walipiga kura katika mfumo wa upigaji kura wa mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.