Pata taarifa kuu
MAREKANI-MDAHALO-SIASA

Trump na Biden watupiana cheche za maneno katika mdahalo usio rasmi

Rais wa Marekani Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wamekuwa wakijibu maswala ya raia wa Marekani kuhusu masuala mbalimbali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 3 Novemba mwaka huu.

Wakati wa mdahlo, Donald Trump na Joe Biden wameendelea kutupiana chche za maneno.
Wakati wa mdahlo, Donald Trump na Joe Biden wameendelea kutupiana chche za maneno. REUTERS/Octavio Jones
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mjini Miami Trump amekanusha kufahamu kuhusu kundi la QAnon linalohusishwa na imani ya kishetani.

"Silijui. Hapana, silijui. Wewe ndiye unayeniambia kuhusu hilo kundi. Lakini nikwambie kile ninachosikia kuhusu kundi hilo ni kwamba wanapingana kwelikweli na wabakaji watoto wadogo na mimi nakubaliana na msimamo wao huo," Trump alimwambia mtangazaji wa ABC.

Biden naye ameendelea kumlaumu Trump kwa kushindwa kutoa uongozi bora wa kudhibiti mamabukizi ya janga la Corona nchini humo.

Akihojiwa na kituo cha televisheni cha ABC mjini Philadelphia, Biden amesema Trump hajayachukulia maradhi hayo, yashayoangamiza Wamarekani zaidi ya 217,000, kwa umakini zaidi.

Wagombea hao waliamua kujibu maswali ya wapiga kura baada ya mdahalo uliokuwa umepangwa kufanyika katika jimbo la Florida, kufutwa baada ya rais Trump kujiondoa.

Katika kile kinachoonekana kama mdahalo baina yao, vituo viwili hasimu vya NBC na ABC nchini Marekani viliwaalika wagombea hao mahasimu pia kwa wakati mmoja kwa mahojiano ambayo yalirushwa moja kwa moja na kwa wakati mmoja usiku wa Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.