Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA

Rais wa Marekani arejea Ikulu siku tatu baada ya kulazwa hospitalini

Rais wa Marekani Doanald Trump ameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kulazwa siku tatu akipokea matibabu baada ya kuambukizwa virusi  vya Corona.

Rais Donald Trump amerejea Ikulu Oktoba 5, 2020.
Rais Donald Trump amerejea Ikulu Oktoba 5, 2020. AP Photo/Alex Brandon
Matangazo ya kibiashara

Madaktari wake wamesema kiongozi huyo wa Marekani anaweza kuendelea kupata matibabu akiwa katika Ikulu ya White House akiendelea na kazi zake.

Baada ya kuwasili katika Ikulu ya White House, Trump alivua barakoa na baadaye kutuma ujumbe akiwataka Wamarekani wasiwe na uoga kuhusu maambukizi hayo, na wasiruhusu yawatawale.

''Nimeondoka kwenye hospitali ya Walter Reed, ni jambo la kipee sana. Nimejifunza mengi kuhusu virusi vya corona. Na jambo moja la uhakika, usiviache viyatawale maisha yako, usiviogope, utavishinda. Tuna vifaa bora kabisa vya matibabu. Na sasa najisikia vizuri. Asanteni sana,'' alisema Donald Trump.

Licha ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini, maswali mengi yameendelea kuulizwa kuhusu hali ya afya ya Trump mwenye umri wa miaka 74, ambaye ni miongoni mwa Wamarekani zaidi ya Milioni 7.4 walioambukizwa virusi hivyo.

Madaktari wake wameonya kuwa bado hajapona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.