Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-UCHAGUZI-SIASA

Kauli ya Trump kuwataka wafuasi wake kupiga kura mara mbili yazua sintofahamu Marekani

Wakati wapiga kura katika Jimbo la North Carolina watapokea kadi zao za kupigia kura kupitia njia ya posta leo Ijumaa, Septemba 4, Donald Trump, rais na mgombea urais wa chama cha Republican, amewashauri wafuasi wake kupiga kura mara mbili, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Donald Trump huko Kenosha, Wisconsin Septemba 1, 2020
Donald Trump huko Kenosha, Wisconsin Septemba 1, 2020 Leah Millis/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Njia mpya ya rais Donald Trump ya kutaka kudhoofisha mfumo wa upigaji kura kupitia njia ya wa posta, ambao anapinga.

Rais huyo mara kwa mara amekuwa akitoa madai ya uongo kwamba kura zinazopigwa kwa njia ya posta zinauwezekano wa kuibiwa.

Wakati uchaguzi wa urais wa Novemba 3 unakaribia, wapiga kura wa Jimbo la North Carolina wanaokadiriwa kuwa milioni 7 watakuwa wa kwanza kupata kura zao kupitia njia ya posta. Kadi hizo zinatarajia kusambazwa Ijumaa Septemba 4.

“Ikiwa una kadi ya kupigia kura kwa njia ya posta, unaituma. Lakini kwa hali yoyote, junguza ... Na nenda kupiga kura! Tuma kadi yako ya kupigia kura mapema, halafu uje kupiga kura. Na ikiwa kura yako bado haijarekodiwa, piga kura, na kura yako itahesabiwa, "amesema Donald Trump.

Wengi wamemshtumu Donald Trump kwa kutoa wito huo kwa wafuasi wake. Mwanamsheria Mkuu wa North Carolina Josh Stein ameandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema kwamba "nimeshtushwa sana na kuwashashawishi " watu katika jimbo "kuvunja sheria ili kumsaidia kupandikiza ghasia katika uchaguzi wetu ".

Msemaji wa bodi ya Uchaguzi ya jimbo la North Carolina ameliambia gazeti la New York Times kwamba katika jimbo hilo haitawezekana kwasababu ni kura ya kwanza pekee itakayorekodiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.