Pata taarifa kuu
MAREKANI-WHO-USHIRIKIANO

Marekani yasitisha mchango wake kwa WHO

Washington imebaini kwamba Marekani haitalipa takriban dola milioni 80 inazodaiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na itatumia pesa hizi kulipa mchango wake wa kawaida kwa Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kuwa Marekani kwa sasa inadaiwa na shirika la Afya Duniani dola Milioni 18 kwa mwaka wa fedha 2019 na dola Milioni 62 kwa mwaka wa fedha 2020.
Mwakilishi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kuwa Marekani kwa sasa inadaiwa na shirika la Afya Duniani dola Milioni 18 kwa mwaka wa fedha 2019 na dola Milioni 62 kwa mwaka wa fedha 2020. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Marekani imepanga kujiondoa rasmi kama mshirika wa shirika la Afya Diuniani, WHO, Julai 6, 2021, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kulishutumu shirika hilo mwezi Mei kuwa ni "kibaraka" wa China tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, tuhuma ambazo shirika hili la Umoja wa Mataifa, lenye makao yake huko Geneva, lilifutilmia mbali.

Kulingana na azimio la pamoja la 1948 katika Bunge la Marekani, Washington inalazimika kutoa muda wa mwaka mmoja juu ya nchi hiyo kujitoa katika WHO na kulipia shirika hilo deni la mwaka wa fedha.

Mwakilishi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kuwa Marekani kwa sasa inadaiwa na shirika la Afya Duniani dola Milioni 18 kwa mwaka wa fedha 2019 na dola Milioni 62 kwa mwaka wa fedha 2020.

"Fedha hizi za pamoja zitapelekwa kwa Umoja wa Mataifa, kulipia mchango wa kawaida wa uanachama katika umoja huo," amesema Nerissa Cook.

Alma Golden, mmoja wa maafisa wa shirika la Marekani la Maendeleo ya kimataifa katika masuala ya afya ya umma, amesema Washington imepata washirika wapya kuendelea na misaada ya kiafya iliyokuwa ikitoa kwa WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.