Pata taarifa kuu
MAREKANI-KENOSHA-MAANDAMANO-MAUAJI-HAKI

Trump kuzuru Kenosha, eneo linalokumbwa na maandamano

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kuzuru mji wa Kenosha, katika Jimbo la Wisconsin, Jumanne wiki ijayo, eneo ambapo Mmarekani mweusi Jacob Blake alijeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi, kesi ambayo imezusha maandamano makubwa nchini Marekani dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Rais Donald Trump, Agosti 29, 2020 wakati wa ziara yake huko Orange, Texas baada ya Kimbunga Laura kupiga Louisiana na Texas.
Rais Donald Trump, Agosti 29, 2020 wakati wa ziara yake huko Orange, Texas baada ya Kimbunga Laura kupiga Louisiana na Texas. AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu Judd Deere ametangaza Jumamosi kwamba Donald Trump atasafiri kwenda Kenosha kaskazini mwa Marekani Jumanne Septemba 1 kukutana kwa mazungumzo na maafisa wa vikosi vya usalama katika eneo hilo na "kutathmini uharibifu uliosababishwa na ghasia "zilizozuka kutokana na kisa hicho.

Jacob Blake, 29, alijeruhiwa vibaya Agosti 23 huko Kenosha wakati maafisa wawili wa polisi walipojaribu kumkamata. Wakati Jacob Blake alipojaribu kuingia ndani ya gari lake, mmoja wa maafisa wa polisi alimpiga risasi saba kulingana na video iliyorekodi tukio hilo.

Akiwa amelazwa hospitalini katika kitongoji cha Milwaukee, katika jimbo la Wisconsin, Jacob Blake amepooza sehemu ya chini ya mwili wake.

Msemaji wa Ikulu ya White House hajabaini ikiwa Donald Trump amepanga kukutana na familia yake wakati wa ziara yake huko Kenosha.

Kesi hiyo, inayokuja baada ya kesi nyingine kadhaa za hivi karibuni za maafisa wa polisi Wazungu kuwafyatulia risasi Watu weusi, imezusha wimbi jipya la hasira na maandamano kote Marekani.

Waandamanaji wenye hasira walikuwa wakipambana na polisi na kuchoma moto magari na majengo.

Wakati huo huo kijana wa umri wa miaka 17 anashikiliwa na mamlaka ya Kenosha kwa kuhusishwa na mashashambulizi ya watu watatu waliokuwa wakiandamana kupinga shambulizi la Blake, ambapo wawili miongoni mwa hao walipoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.