Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Marekani: Trump amshambulia Biden baada ya kuridhia uteuzi wa chama cha Republican

Rais wa Marekani Donald Trump amekubali uteuzi wa chama chake cha Republican kuwa mgombea urais kwa muhula wa pili katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Novemba 3, baada ya Mkutano mkuu wa chama chake kumpitisha.

Donald Trump ameridhia uteuzi wa chama cha Republican kwa kuwania katika uchaguzi wa urais katika hotuba alitoa Ikulu ya White Agosti 27, 2020.
Donald Trump ameridhia uteuzi wa chama cha Republican kwa kuwania katika uchaguzi wa urais katika hotuba alitoa Ikulu ya White Agosti 27, 2020. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake, Donald Trump amemshambulia mpinzani wake katika uchaguzi huo, Joe Biden, mgombea wa chama cha Democratic, akidai 'atasababisha Marekani kudorora kiusalama na kiuchumi' ikiwa atachaguliwa.

"Huu ni uchguzi muhimu zaidi katika historia yetu," ameonya Donald Trump, "chaguo kati ya Marekani mbili. Yake, anayosema kama ile yenye usalama wa kutosha, au ile ya machafuko ikiwa chama cha Democratic kitashinda, ambacho kitawakilishwa na Joe Biden, 77, ambaye Trump anasema ni kibaraka wa mrengo wa kushoto.

Wakosoaji wa Rais Trump wamekuwa wakimkosoa kwa kusema amekuwa chachu ya vurugu. Pamoja na Marekani kuzongwa kwa hali ya ubaguzi wa rangi, bado pia taifa hilo lipo katika makabiliano ya virusi vya Corona.

Donald Trump amesema yeye ndie rais bora kuwahi kushuhudiwa toka zama za Abraham Lincoln ambae alifanikisha taifa kujiondoa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kokomesha biashara ya watumwa. Hata hivyo aliendelea kutoa ahadi kama atafanya vizuri zaidi endapo atachaguliwa katika uchaguzi ujao. Alisema amefanya mengi zaidi katika kipindi chake cha miaka minne ikilinganishwa na hasimu wake Joe Biden ambae amekuwepo katika siasa kwa miaka 47.

Uchaguzi nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba 3, 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.