Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAANDAMANO-USALAMA

Marekani: Maandamano yatanda Wisconsin baada ya polisi kumpiga risasi mtu mweusi

Sheria ya kutotoka nje imetangazwa huko Wisconsin, nchini Marekani baada ya polisi kumpiga risasi kadhaa mtu mweusi, hali ambayo imezusha maandamano makubwa katika eneo hilo.

Tukio hilo limeibua mjadala mwingine baada ya matukio kama hayo kutokea siku za nyumba nchini Marekani, hususan lile la George Floyd, Mmarekani mweusi, mwenye umri wa miaka 46, aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi Mei 25 mwaka huu.
Tukio hilo limeibua mjadala mwingine baada ya matukio kama hayo kutokea siku za nyumba nchini Marekani, hususan lile la George Floyd, Mmarekani mweusi, mwenye umri wa miaka 46, aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi Mei 25 mwaka huu. REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wanasema Bwana Blake alipigwa risasi mgongoni wakati aalikuwa anajaribu kuingia kwenye gari lake katika mji wa Kenosha.

Tukio hilo limeibua mjadala mwingine baada ya matukio kama hayo kutokea siku za nyumba nchini Marekani, hususan lile la George Floyd, Mmarekani mweusi, mwenye umri wa miaka 46, aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi Mei 25 mwaka huu.

Maafisa wa usalama wenye itikadi za ubaguzi wa rangi wamekuwa wakinyooshewa kidole cha lawama kuhusika na visa mbalimbali vinavyohusiana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Wamarekani weusi nchini humo.

Jacob Blake, amelazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya, amesema Gavana wa Wisconsin, Tony Evers.

Video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii na ambayo iliyorushwa hewani na vyombo vya habari vya Marekani inaonyesha mtu akieelekea gari lake huku, akifuatwa na maafisa wawili wa polisi. Mmoja wa maafisa hao wa polisi anaonekana akimpiga risasi nyingi wakati mtu huyo alipokuwa akifungua mlango wa gari.

Picha hizo zimezusha hasira katika mji huo wa Marekani. Kulingana na picha za mitandao ya kijamii, umati wa waandamanaji wamemiminika mitaani huko Kenosha na kuwarusha mawe na machupa maafisa wa usalama.

Wakati huo huo polisi imetangaza sheria ya kutotoka nje katika mji huo hadi saa 7:00 asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.